ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 3, 2015

JANUARY MAKAMBA AFUNGUKA KUHUSU VIKATUNI VYA INSTAGRAM

Jeh katuni hii ilikuwa na maana gani?
Na hii jeh?
Mtu aliyetupwa kwenye shimo lenye baridi kali, kisha akatupiwa ngazi ili kuokolewa lakini cha ajabu alikata vipande vya ngazi hiyo na kuvikoka moto ili kupata joto.
Maswali mengi yamezuka yakiambatana na tafsiri zake mara baada ya posti hizi  kuonekana katika ukurasa wa akaunti ya Intsgramu ambayo inasadikika kuwa ni ya Mhe. January Makamba ambaye alikuwa naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia, Mbunge wa sasa wa Jimbo la Bumbuli (CCM).

Wachambuzi mbalimbali wamezitafsiri katuni hizo kuwa zinaubeza utawala wa Rais wa awamu ya Tano Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli. Baada ya kimya cha majibu kuhusu vikaragosi hivyo, kituo cha radio chenye maskani yake jijini Mwanza, Jembe Fm kupitia kipindi chake cha KAZI NA NGOMA kiliamua kumtafuta Mhe. January Makamba na kutatua utata ulio kuwako. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.