Hati ya malipo kwa ajili ya vipimo vya MRI kwa dada Joyce iliyotolewa leo baada ya kulipiwa. Inatarajiwa atapimwa Alhamisi ama Ijumaa kabla jopo la Madaktari kuamua nini cha kumfanyia. |
UPDTAES ZA LEO
Kwa kutumia michango ya wasamaria wema, leo tayari Ankal ameshalipia malipo kwa ajili ya vipimo vya MRI kwa dada Joyce yanayotarajiwa kufanyika Alhamisi hii ama Ijumaa. Baada ya matokeo ya vipimo vyake jopo la madaktari bingwa bingwa litakaa nakuamua nini cha kufanya kumsaidia dada Joyce. Hivyo tuendelee kumsaidia kwa hali na mali pamoja na dua.

Kama umeguswa na unataka kutoa msaada unaweza kuwasiliana na Ankal kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba+255 754 271266 kwa jina la Ankal.
AU mratibu-mwenza Deo Kakuru Msimu
Pia unaweza kuwasiliana moja
kwa moja na dada Joyce kwa namba hiyo na atafurahi
ukimsalimia ama hata kumtupia kitu kwenye Mpesa yake.
MPIGIE +255 768 084897
kwa moja na dada Joyce kwa namba hiyo na atafurahi
ukimsalimia ama hata kumtupia kitu kwenye Mpesa yake.
MPIGIE +255 768 084897
-----------------------------------------
HISTORIA YA MATATIZO YA DADA JOYCE
HISTORIA YA MATATIZO YA DADA JOYCE
Ifuatayo ni historia fupi ya matatizo ya dada
Joyce Richard Mwambepo, mkaazi wa kitongoji cha Sinde jijini Mbeya mwenye umri wa miaka 27 ambaye anaishi
na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na mwanaye mwenye umri wa miaka 4.
Ikumbukwe kuwa mwezi wa nne (April) mwaka jana dada huyu aligongwa na gari ambalo dereva wake hakusimama kumsaidia. Wasamaria wema walijitokeza na kumpelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya ambako alikaa wodini kwa miezi mitatu bila kupata matibabu kwa kukosa fedha.
Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili, hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi lakini nako huko pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa Mbeya kwa kukosa pesa za matibabu.

Akajitokeza mwanahabari Deo Kakuru wa Mbeya ambaye baada ya kumgundua alitoa taarifa za
dada Joyce katika mitandao mbalimbali, ambapo wasamaria wema wengi wa ndani na nje ya nchi wakaguswa na kuchangia.
Mungu mkubwa, kiasi kilichopatikana ( 3.2m/-) kimewezesha dada Joyce kupelekwa Dar es salaam toka Mbeya kwa ndege ya Fast Jet Alhamisi iliyopita na moja kwa moja kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alipokelewa katika kitengo cha mifupa cha MOI na kupatiwa kitanda katika wodi mpya ijulikanayo kama Wodi ya Magufuli, ghorofa ya tatu wodi namba 2 chumba cha kwanza kulia.

Cha
kufurahisha ni kwamba Joyce aliweza kukaa kwenye kiti cha kusukumwa na hata
kwenye ndege aliketi kama kawaida, zoezi ambalo hata yeye anasema limemsaidia
kwani kwa mara ya kwanza hivi sasa ganzi miguuni inapotea taratibu na ukimgusa
anahisi mguso tofauti na ilivyokuwa awali.
Daktari
bingwa ameshaonana naye na kumpa matumaini ya kupona, hasa sehemu ya chini ya
uti wa mgongo wake ambao inasemekana una matatizo yaliyopelekea kubana mishipa ya fahamu na kufanya miguu ipooze.
Zoezi linalosubiriwa kwa sasa ni kupatiwa vipimo vya MRI ili kubaini kiufasaha
tatizo lake na hatimaye kupatiwa matibabu. Zoezi hili linatarajiwa kufanyika
wakati wowote kuanzia sasa.
Mpiganaji
Deo Kakuru amesharejea Mbeya na kijiti cha kumwangalia dada Joyce amekabidhiwa
Ankal ambaye anaomba Wasamaria wema waendelee kumuombea na kumsaidia kwa hali
na mali dada huyu ambaye ni yatima.
Kwa bahati njema
Ankal amekutana na kuongea na Msamaria mwingine aitwaye Mama Rozi ambaye anamuuguza mama yake mzazi aliyelazwa wodi moja na dada Joyce. Msamaria huyu
amekubali kumsaidia dada Joyce kwa chakula na pia kumsaidia usafi maana hapo
kitandani alipo hawezi kuondoka...Hivyo mambo yote anamalizia hapo hapo.
Mungu kweli ni
mkubwa. Dada Joyce anatabasamu na kuongea vizuri tu. Anatoa shukurani sana kwa
wote waliomsaidia na wanaoendelea kumsaidia. Anasema hana cha kuwalipa ila kusema
ASANTE SANA na anamwomba Mola Muumba awazidishie pale patapopungua. Ameomba
anayeweza kumtembelea afanye hivyo na atafurahi sana maana hana ndugu hapa Dar es salaam zaidi ya Ankal.
Pia anawashukuru sana madaktari waliomhudumia vyema katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ambao amesema hatowasahau kwa msaada wao mkubwa waliompa wakati wa kupata ajali na huu.
Dada Joyce pia anawashukuru sana Dkt Hellen na Dkt Mtei ambao amesema wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba huduma anazopata hapo MOI ni zitamsaidia kupata matibabu yake.

Dada Joyce akiwa ameketi kwa utulivu kwenye siti yake ndani ya ndege wakati wa safari ya kutoka Mbeya kuelekea Dar es salaam.
Mpiganaji Deo Kkuru akiwa na dada Joyce mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam
Msamaria mwema Mama Rozi akimhudumia dada Joyce akiwa kitandani kwake Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa cha MOI katika wodi ijulikanayo kama Wodi ya Magufuli ghorofa ya tatu
Dada Joyce akiwa wodini Moi
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.