ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 16, 2015

WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB WAKISHIRIKI MICHEZO MBALIMBALI KATIKA SIKU YA FAMILIA YA CRDB.


 Wafanyakazi wa  Benki ya CRDB mkoa wa Arusha  wakishindana kuvuta kamba
katika viwanja vya Olasiti Garden leo katika sherehe za siku ya familia ya
CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi
wa benki pamoja na familia za wateja.
 Watoto wakifurahia michezo mbalimbali   katika viwanja vya Olasiti Garden
leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka
na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za
wateja.
 Wafanyakazi wa  Benki ya CRDB mkoa wa Arusha  wakishindana kuvuta kamba
katika viwanja vya Olasiti Garden leo katika sherehe za siku ya familia ya
CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi
wa benki pamoja na familia za wateja.
 Watoto wakifurahia michezo mbalimbali   katika viwanja vya Olasiti Garden
leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka
na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za
wateja


Meneja wa Benki ya  CDRB  tawi la Usa River  lilipo mkoani Arusha  Jenipher
 Tond akikabidhi zawadi ya tisheti kwa mtoto aliyeshinda kucheza mziki
leo sherehe a siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja

 Watoto wakimkimbiza kuku katika mashindano yaliyofanyika kwenye sherehe za
siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na
familia za wafanyakazi wa benki pamoja na familia za wateja
 Malindi band ya mkoani kilimanjaro ikitumbuiza sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafanyakazi wa benki pamoja na familia za wateja
Mfanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la USA akikabidhi zawadi kwa mtoto
 Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
Benki ya CRDB imeendelea kukuza kipato cha familia nyingi nchini za hali ya chini, kati na juu kwa kuwahimiza wateja wake kufanya uwekezaji wenye tija pamoja na kujiwekea akiba kwa maisha ya baadae.

Hayo yameelezwa Meneja wa Benki ya  CDRB  tawi la Usa lilipo mkoani Arusha  Jenipher Tond wakati wa maadhimisho ya siku ya Familia ya CRDB iliyofanyika katika viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha na kuzikutanisha familia mbalimbali za wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na familia za wateja wa benki hiyo waishio jijini Arusha.

Meneja huyo amesema kuwa benki hiyo inaendelea kuhamasisha uwekezaji na
kutoa mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji na kuinua pato la mwananchi mmoja mmoja hadi kwa taifa.

Meneja wa benki hiyo tawi la Meru Leonce Mathey amesema kuwa benki hiyo
imesogeza karibu huduma kwa wananchi ikiwemo boda boda ,mama ntilie pamoja
na wajasiriamali kwa kuanzisha matawi katika maeneo ya masoko .

Leonce amewataka wafanyakazi wa CRDB kutumia vyema siku familia  kwa kukaa
karibu na familia zao na kufurahi pamoja kwani muda mwingi wanautumia katika kufanya kazi za kuwaingizia kipato .

“Kama kwenye familia mambo hayako vizuri nyumbani hata kazini mambo  hayatakua
vizuri ni vyema kuhakikisha mazingira yanakua mazuri kuanzia kwenye familia mpaka kazini” Alisema Leons

Kwa upande wake Mteja wa benki hiyo Pendo Shoo amesema kuwa benki hiyo
imemsaidia kuwalipia watoto wake ada kupitia akaunti ya Junior Acount ambazo huwawezesha pia kupata mikopo kwa ajili ya kuwaendeleza watoto kielimu.

Benki ya CRDB  ina matawi 8 na matawi mengine madogo madogo bado yataendelea kuanzisha ili kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi.

Siku ya familia ya CRDB iliambatana na michezo   na burudani  ambazo zilipamba siku hiyo ikiwemo mchezo wa kuvuta kamba ,kukimbia na yai mdomoni pamoja na burudani ya muziki .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.