ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 5, 2015

UVAMIZI SHINYANGA.

Na Emmanuel Mlelekwa,
Novemba 5,2015.
KAHAMA.

Watu wawili Bakari Hamis (45) na Abraham Hamis(24) wote wakazi wa Nyasubi wilayani Kahama mkoani Shinyanga usiku wa kuamkia leo wamejeruhiwa kwa kukatwa na vitu vyenye nchakali katika miili yao na watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi.

Tukio hilo limetokea  majira ya saa 8 za usiku ambapo kwa mujibu wa Mashuhuda wamesema watu hao ambao idadi yao haikufahamika walitumia Nondo na Mawe kuvunja nyumba  ya mfanyabiashara Bakari akiwa na mdogo wake na kisha kutekeleza tukio hilo.

Mmoja wa Mashuhuda hao Miraj Shaban amesema alisikia sauti za nyumba ya jirani yake ikivunjwa ndipo alipoamua kufuatilia ambapo tayari watu hao walikuwa wameshafanya  tukio hilo na kukimbia ndipo alipooa taarifa Polisi ambao walifika baada ya nusu saa.

Akielezea tukio hilo Bakari Hamis amesema kuwa watu hao waliingia na kumwamuru atoe fedha na alipokaidi wakaanza kuwashambulia yeye na mdogo wake kwa kutumia vitu vyenye ncha kali na kisha kuwapora simu na kukimbia.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Kahama Joseph Ngowi amesema ofisi yake imewapokea majeruhi hao na kuwapatia Matibabu huku hali zao zikiendelea vizuri na muda wowote wanaweza kuruhusiwa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga  Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa upelelezi unaendelea kuwabaini waliohusika ili sheria ichukue mkondo wake dhidi yao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.