Novemba 6,2015.
KAHAMA
Kuelekea msimu mpya wa kilimo Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga imewataka wakulima kutumia Pembejeo zinazosambazwa na Mawakala waliothibitishwa na Serikali badala ya kununua mtaani.
Akizungumza na Jembe Fm Kaimu Afisa Kilimo wa Halmashauri hiyo Mshana Wilson amesema kuwa Serikali imepanga kuboresha kilimo cha Wakulima kwa kuleta Pembejeo bora ambazo zitakuwa na tija kwa wakulima.
Mshana amesema kuwa Wakulima wanatakiwa kutumia Pembejeo zinazosambazwa na serikali kwa mfumo wa Vocha na tayari usambazwaji wake umeanza kwa utaratibu maalum kupitia ofisi za kata.
Ameongeza kuwa Halmashauri hiyo imepata Vocha ya Pembejeo za Mahindi na Mpunga kwa upande wa mazao ya Chakula, Pamba na Tumbaku kwa upande wa Biashara pamoja na Mbolea na Madawa ambazo zitagawiwa kwa wakulima.
Hata hivyo takwimu sahihi ya idadi ya wakulima watakaopatiwa Pembejeo hizo bado haijafahamika sanjari na gharama ya vocha ya Pembejeo hhizo kutokana na Mawakala wa usambazaji kutowasilisha nakala hadi sasa kwa Mkurugenzi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.