Mbunge viti maalumu kupitia Wazazi Phide Mwakitalima ambaye naye aliongozana na vijana hao katika kuhamasisha kumchagua kiongozi anaefaa kuongoza jiji la Arusha na kuleta maendeleo
Mbunge wa viti maalumu Phide mwakitalima akiwa anamuamasisha mmoja wa mfanyabishara kuchagua kiongozi anaefaa siju ya october 25
Habari picha na Woinde Shizza, Arusha
Wananchi wa mkoa wa Arusha na vitongoji vyake wametakiwa kukataa mihemko ya kampeni za
uchaguzi ili isiwe chanzo cha kuwagawa na kuwagombanisha wao kwa wao
kwani kuna maisha baada ya uchaguzi.
Hayo yamebainishwa na
baadhi ya vijana kutoka katika vyama mbalimbali vya siasa mkoani Arusha
wakati walipokutana kuzungumzia hatma ya jimbo lao la Arusha mjini .
walisema
kuwa kwa mkoa wa arusha kumekuwa na mhemko ya siasa ambayo imewatawala
sana vijana hali ambayo inapelekea uvunjifu wa amani na hata kuleta
ugomvi .
Mmoja wa vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la
Sauli Melayeki ambaye alitokea katika kata ya Olasiti alisema kuwa ni
wajibu wa kila mwananchi kuachana na miemkoa ya kisiasa na kutambua
kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.
Alisema kuwa imefikia
wakati vijana kukaa chini na kutafakari na kufanya siasa zamsingi na
kuacha siasa za ushabiki ambapo zinapekea kuchagua kiongozi mradi
kiongozi bila hata ya kumuangalia kama ana faa au hafai.
Alisema
kuwa kwa kipindi hichi wananchi wa jiji la arusha wanatakiwa wakae
chini wafanye tasimini wawaangalie viongozi wote kutoka vyama vyote
ambao wanagombania nafasi mbalimbali za uongoz i wakianzia wabunge
pamoja na madiwani wao waaangalie uelewa wao au kama watafakuwaongoza na
kuweza kukuwawakilisha vyema wananachi wao katika sehemu husika na sio
wale viongozi ambao watakuwa wanasababisha uvunjifu wa amani.
kwaupande
wa kijana mungine aliyejitambulisha kwa jina la Anna Mwambapa alisema
kuwa wananchi wajitaidi kufanya siasa za amani zisizoleta chuki
,machafuko pamoja na uvunjifu wa amani na iwapo vitu hivyo vitatokea
basi wamama na watoto pamoja na wananchi kwa ujumla watapata shida sana.
Aidha
alibainisha kuwa mkoa wa huu na jiji kwa ujumla umepoteza muelekeo
kabisa katika kipindi kilichopita kwani kiongozi waliomchagua akuwa
muadilifu akutekeleza ahadi yeyote ambayo aliwahaidi hususa ni wao kama
wafanya biashara na badala yake amesababisha wao kama wafanyabiashara
kunyanyanyasika pamoja na kuteseka kwani aliwahaidi kuwatengea sehemu ya
kufanyia biashara lakaini ajafanya hivyo adi sasa wamekeuea wakifukuzwa
kila siku kama wakimbizi.
"mimi naomba tuwe makini sana
kuchagua kiongozi katika kipindi hichi na tusifanye kosa kama kipindi
cha nyuma tulivyofanya kosa kwa kumchagua mtua ambaye kila siku amekuwa
anafanya maandamano alituahadi wafanyabiashara mengi lakini amna ata
moja alilolitekeleza badala yake amekuwa ni mtua ambaye atumuelewei
"alisema Mwambapa
Aliongeza kuwa ni wakati wa kila
mwananchi kumchagua kiongozi ambaye anafaa kiongozi ambaye anania na
kiongozi ambaye anawajali wananchi wake na yule ambaye atawathamini kwa
kutekeleza ahadi ambazo amewahaidi wananchi wake.
Vijana hao waliamua kutembelea pia soko la kwa morombo ili kuweza kuwahamasisha wafanyabiashara kuchagua kiongozi anaefaa siku ya tarehe 25
baadhi ya vijana hao wakiwa wanaonyesha hisia zao
Pia kulikuwa na mechi walioiyandaa yote haya yalikuwa ni kuamasisha kumchua kiongozi ambaye anaeweza kuibadilisha mkoa wa Arusha pamoja na kata zake
Hapa baadhi ya vijana waliamua kupiga push shap huku wakisema hapa kazi tu
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.