Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa(CCM) Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta juzi katika pori la akiba la mbuga ya Selous. Marehemu aliagwa katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.PICHA NA MICHUZI JR.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimfariji Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe akilia kwa uchungu kufuatia kifo cha Mumwe Deo Filikunjombe,wakati wa kuaga katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
Dkt Magufuli akifarijiana na Mh.Zitto Kabwe wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
Dkt Magufuli alishindwa kujizuia kutoa machozi ya huzuni wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
Majeneza yenye miili ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deogratias Filikunjombe na ndugu zake, Plasdus Ngabuma na Casablanga Haule yakiwa yamewekwa mbele ya waombolezaji wakati wa kuaga katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. kabla ya kusafirishwa kwenda Ludewa kwa mazishi mkoani Njombe.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.