ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 17, 2015

MWANZA YAAHIDI KUMPA KURA ZA NDIYO MAGUFULI :- AWANADI VYEMA WAGOMBEA UBUNGE ILEMELA NA NYAMAGANA.

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.John Pombe Magufuli akimwaga sera kwa wananchi waliofurika kwa wingi kwenye mapokezi yake jijini Mwanza, na hapa alikuwa akitokea uwanja wa ndege wa Mwanza kuelekea viwanja vya furahisha ambako ndiko shughuli nzima ilifanyika.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kwa wananchi waliojitokeza kumpokea.
Watu na mtu wao.....
Sasa ni safari kutoka airport Mwanza hadi viwanja vya Furahisha vilivyoko Kirumba jijini Mwanza.
Barabara ya Makongoro jijini Mwanza.
Watu wamefurika hapa.
Ni upenyo almuradi kupata kuona kile kilichokuwa kikifanyika.
Katika mkutano huo Dkt.Magufuli alipata mapokezi makubwa kiasi cha kuuufanya Uwanja wa Furahisha kuelemewa na idadi ya wananchi na Makada wa CCM waliofika uwanjani hapo.
Katika mkutano huo Dkt.Magufuli alipata mapokezi makubwa kiasi cha kuuufanya Uwanja wa Furahisha kuelemewa na idadi ya wananchi na Makada wa CCM waliofika uwanjani hapo.
Akizungumza katika Mkutano huo,Dkt. Magufuli alishindwa kuficha hisia zake na kueleza kuwa Mwanza wamejitokeza kwa wingi sana kiasi cha kufanya idadi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo kutofikiwa na idadi yoyote ya wananchi waliojitokeza katika mikutano ya kisiasa barani Afrika.
Katika hotuba yake Dkt.Magufuli alisisitiza kwamba hatawaangusha watanzania ikiwa watampa ridhaa ya kuwa rais wao katika Uchaguzi Mkuu ujao unaotarajia kufanyika Octoba 25 mwaka huu na kuongeza kuwa atahakikisha anasimamia vyema shughuli za maendeleo ikiwemo kufufua viwanda vilivyobinafsishwa na havifanyi kazi, kutoa elimu kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne pamoja na kuondoa kero ya ushuru inayowakabiri watanzania hivi sasa
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Dkt.Antony Diallo akizungumza katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza kwenye mkutano wa hadhara wa kuomba kura kwa wananchi katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu nchini.
Ikiwa ni kwa ajili ya maendeleo yao, dkt.Magufuli aliwaomba watanzania kuwachagua viongozi wanaotokana na CCM Kuanzia ngazi ya Madiwani, Wabunge na Rais ambapo aliwatambulisha wagombea mbalimbali Mkoani Mwanza akiwemo Stanslaus Mabula ambae ni mgombea ubunge Jimbo la Nyamagana (kulia) pamoja na Angelina Mabula ambe ni Mgombea ubunge jimbo la Ilemela (kushoto)
Magufuli ameomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi huku akiahidi kuwa iwapo wananchi wakimchagua kuwa rais wa awamu ya tano atakuwa kufuli la kufunga milango na upenyo wa mianya yote ya rushwa na ufisadi katika idara mbalimbali za serikali.
Angelina Mabula ambe ni Mgombea ubunge jimbo la Ilemela.
Stanslaus Mabula ambae ni mgombea ubunge Jimbo la Nyamagana.
Bango lasomeka hivi.
Wananchi wakipunga mikono hewani kuashiria maridhiano na kile kilichokuwa kikiendelea jukwaa kuu.
Wananchi wakisikiliza sera katika Uwanja wa Furahisha kwenye mkutano wa hadhara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt.John Pombe Magufuli wa kuomba kura kwa wananchi katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu nchini.
Watu na vyama vyao....watu na watu wao.
Ni katika Uwanja wa Furahisha kwenye mkutano wa hadhara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt.John Pombe Magufuli wa kuomba kura kwa wananchi katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu nchini
Wananchi waliofurika kusikiliza sera kwenye mkutano wa hadhara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt.John Pombe Magufuli wa kuomba kura kwa wananchi katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu nchini.
Wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM zilizohudhuriwa na Maelfu ya watu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.