ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 17, 2015

Uchaguzi Guinea:Alpha Conde aongoza


Image copyrightAFP
Image captionAlpha Conde
Matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Guinea yanaonyesha kuwa rais wa sasa Alpha Conde ameshinda kura za kutosha kuzuia kuwepo duru ya pili ya uchaguzi.
Huku asilimia 90 ya kura zikiwa zimehesabiwa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo inasema kuwa bwana Conde yuko mbele ya mshindani wake mkuu Cellou Dalein Diallo.
Image copyrightAFP
Image captionCellou Dalein Diallo.
Kiongozi huyo wa upinzani alisema wiki iliyopita kuwa alikuwa anajiondoa kwenye uchaguzi huo akidai kuwepo udanganyifu.
Uchaguzi huo ulifanyika licha ya janga la hivi majuzi la ugonjwa wa ebola ambalo liliwaua maelfu ya watu. CHANZO BBC SWAHILI.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.