ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 14, 2015

DK MAGUFULI AOMBWA KUSHUGHULIKIA UJENZI WA BARABARA, MAJI NA NYUMBA ZA WATUMISHI WA SERIKALI JIMBO LA ITILIMA

Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli, akimkabidhi ilani ya ya uchaguzi CCM, mgombea ubunge wa jimbo la Itilima Njalu Silanga alipokuwa akiomba kura kwa wananchi na kumnadi mgombea huyo.
Na PETER FABIAN, ITILIMA

MGOMBEA  Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli, amempongeza mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Itima, Njalu Silanga, kwa kuanza kuomba kwake akishinda uchaguzi wa nafasi hiyo aanze kushughulikiwa kero na matatizo ili kumaliza matatizo ya wananchi.

Magufuli alisema kwamba kitendo cha mgombea Ubunge, Silanga kutambua majukumu yake ya kuwatumikia wananchi kabla hata ajachaguliwa ni ishara nzuri ya kuonyesha dhamira yake ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo ambalo limekuwa chini ya upinzani kwa miaka 15 likiongozwa na John Cheyo (UDP).

"Wananchi wa jimbo hili nichagulieni huyu kijana kwani ameonekana atanisaidia sana kwa kuwa ameonekana kuwa mgombea aliye na maono ya mbali, lakini pia upeo wake wa kuwatumikia umeanza kuonekana hata kabla ya kumchagua hivyo msifanye makosa kuniletea ili tufanye kazi za uhakika,"alisisitiza

Naye mgombea  Ubunge Silanga, amemuahidi maendeleo makubwa mgombea urais wa Chama hicho, Dk Magufuli iwapo watachaguliwa na wananchi kuliongoza taifa kwa miaka mitano ijayo kwa kuwa ni mtu wa kazi na ufatiliaji.
  
Silanga ameahidi, iwapo Dk Magufuli anataka ‘kazi tu’ yeye atakuwa ni mbunge wa ‘vitendo tu’ ili maendeleo ya wananchi wa wilaya hiyo mpya yapae.
 
Majibu ya ahadi hiyo iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita (jumamosi) kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM katika Kijiji cha Nanga wilayani humo, yalipotolewa na Dk Magufuli yalikonga nyo za mamia ya wananchi hao waliopaza sauti kuomba wambebe huku wakiwaahidi kura za kishindo.
 
Mgombea ubunge wa jimbo la Itilima Njalu Silanga akipongezwa na Raphael Chegeni (mgombea ubunge jimbo la Busega) kushoto ni Mjumbe wa timu ya kitaifa ya Kampeni na Mgombea ubunge jimbo la Bunda Stephen Wasira.
“Mheshimiwa mgombea urais Dk Magufuli najua wewe ni kipenzi cha wananchi wengii na wagombea wengine wanashiriki uchaguzi tu, mimi tayari nakuita Rais mteule..” alisema Silanga na kuufanya umati wa wana Itilima uzizime kwa shangwe na kukubaliana naye kuwa huyo ndiye rais wanayemhitaji awamu ijayo.
 
“Hapa yapo matatizo makubwa ya barabara, maji safi na salama ya kunywa, mabwawa na malisho ya mifugo wetu, tunajua wewe ni mtu wa sheria uje ulishughulikie hilo watu wanateseka hawana marisho, watumishi hawana nyumba,” aliomba mgombea huyo.
 
Silanga ambaye aliahidi pia kuboresha huduma za jamii na kuwapiga jeki vijanan, alifafanua kuwa, wananchi wa wilaya hiyo wamekosa malisho ya mifugo kwa sabau ya mgogoro ulioshindikana kutatuliwa baina yao na pori la hifadhi ya akiba ya Maswa, hivyo wanaamini atakapokuwa rais kero hiyo itatatuliwa mara moja.
 
Mgombea huyo alimpongeza Rais Dk Jakaya Kikwete kwa kuansisha wilaya hiyi ili kusogeza karibu huduma za wananchi na kuondoa michango mbalimbali iliyokuwa kero kwa wananchi na sasa CCM imepania kutoa elimu ya msingi hadi kidatro cha nne bure.
 
Akijitambulisha na kuomba wana Itilima wampe kura za kishindo, Dk magufuli alimfagilia Silanga kwa kumuahidi kutekeleza kwa vitendo Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 ambayo itataua kero hizo.
 
“Barabara zenu na daraja nimeziona, nawaahidin ndugu zangu nikiwa Rais nitayatekeleza na kuijenga wilaya hii mpya ikiwa pamoja na nyumba za watumishi, suala la mpaka nitalishughulikia maramoja mpate malisho,” alisema.
 
Alihoji, atashindwaje suala la mipaka ya ardhi akiwa rais wakati rais ndiye mwenye mamlaka ya kubadilisha matumizi ya ardhi, na kuwafanya tena wananchi hao wamshangilie na kumuomba kwa lugha ya kisukuma wambebe (kama heshima) na ishara ya kutukuka.
 
“Mnataka kunibeba ?” walimjibu “Ndiyo” Dk magufuli akawashukuru na kuwaomba wambebe kwa kumpigia kura za ndiyo nyingi ikiwa pamoja na wagombea wote wa udiwani na ubunge wa CCM, wasipofanya hivyo hata kama wakimbeba mgongoni haina maana na matumaini yao yatapotea bure.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.