ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 24, 2015

AIRTEL YAZINDUA KIFURUSHI CHA 'YATOSHA NYTs'

Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde (kulia) na Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki wakionyesha bango kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kama ishara ya kuzindua huduma mpya ya kifurushi cha ‘Yatosha Nyts’ itakayomwezesha mteja kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo pamoja na kupata kifurushi cha internet cha MB 10 kwa kiwango cha shilingi 300 tu. 


Airtel yazindua kifurushi cha “Yatosha Nyts” bila kikomo · 

Wateja kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi bila kikomo· Piga simu bure kila siku kuanzia saa 5 usiku mpaka 12 asubuhi ·

 Kwa shilingi 300 tu. Dar es Salaam,Jumatano 23 Septemba 2015, Kampuni ya simu za mikononi Airtel imewapa sababu nyingine wateja wake kufurahia usiku kwa kuwapatia “Yatosha Nyts” ofa inayowawezesha kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo,pamoja na kifurushi cha internet cha MB 10 kwa kiwango cha shilingi 300 tu.

Ofa hii ya “Yatosha Nyts” inawawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) kwenda mitandao yote kila siku kuanzia saa 5 usiku hadi saa 12 asubuhi hadi siku za wikiendi.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde alisema, “ Tunatambua wateja wetu wanamahitaji tofauti ya huduma za simu. “Yatosha Nyts” ni ofa kabambe na ya kipekee inayo kidhi mahitaji ya wateja wetu. Tumezindua “Yatosha Nyts” ofa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja wetu ya kuwasiliana na kupanga shughuli za siku inayofuata bila hofu ya kupungukiwa na salio kwenye simu zao.

 “Yatosha Nyts” inawawezesha wateja kuwasiliana na familia, marafiki , mpenzi na wafanya biashara wenzake wakati wa usiku kwa bei nafuu zaidi.

Aliongeza kwa kusema, “ikiwa ni mwendelezo wa kutoa huduma za mawasiliano bora zenye gharama nafuu, wateja wetu wanauwezo wa kununua kifurushi cha “Yatosha Nyts” wakati wowote na kuanza kufurahia kupiga simu, kutuma SMS bila kikomo na 10MB za kuperuzi.

Kwa shilingi 300 tu wateja wetu nchi nzima wanaweza kupiga simu bila kikomo Airtel kwenda Airtel , kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo kwenda mitandao yote na 10 MB za kuperuzi katika mitandao ya jamii kila usiku. Kujiunga na “Yatosha Nyts” piga *149*99#, “Yatosha Nyt” ni offa mpya na moja kati ya ofa nyingi zenye ubora ambazo Airtel inawatapia wateja wake chini ya huduma ya kibunifu ya Airtel Yatosha.

Airtel Yatosha inawapatia wateja wetu uhuru wa kununua kifurushi kinachowafaa kupitia huduma ya Airtel Money au kwa kutembelea sehemu za kutoa huduma.

Yatosha pia inawawezesha wateja kutengeneza kifurushi wanachokipenda, huduma ya kibunifu na ya kwanza kutoka Airtel

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.