AINA ZA WATU KWENYE GRUPU ZA WATSAPU.
1. VISOKOLOKWINYO - hawa ni aina ya watu ambao kamwe hutawakosa online. Chochote kisemwacho lazima mchango wake autie.
2. VIPWINTO - hawa ni aina ya watu ambao hawajibu comments kabisaaaa, yeye ukimsifia huko aliko anacheka hadi jino la mwisho ila kujibu utangoja. Kisha wanakukujia kwa inbox kukushukuru..eti 'Hapo sasa..'
3. VIPOCHI MANYOYA - hawa ni aina ya watu ambao wao hutukana kuanzia asubuhi hadi jioni bila kuchoka wala kukata tamaa, yaani kila anacho comment kama sio kukera basi tusi.
4. MWAITAKOTAKO - hawa ni aina ya watu ambao kazi yao nikubadilisha profile picture ya grupu na wakicomment wao husema tu 'following'
5. VISHKWAMBI - hawa ni aina ya watu flani amaizing, hawanaga tatizo na mtu, wanajibu comments alafu hawana matusi.
6. KAPWEPWE - hawa ni aina ya watu ambao watacomment only when mtu flani ata posti cho chote kile. Hao hucomment ata kama huyo mtu ajaposti.. Bora waone tu '....is typing'
7. VITWEYA - Hawa niwa aina ya kipekee. Ni mashujaa wa kueneza umbea. Kazi zao niku screeni shoti nakusambaza siri za grupu na chochote kile kinacho changiwa na washikadau wa grupu.
8. MABUDEDE - Wapewe saluti...! Hawa wenzetu hawalali ng'oo. Wapate faragani usiku kucha. Wanapenda kuchati masaa ya usiku wenzao wakiwa usingizini. Asubuhi ukiamka notifikesheni chungu nzima.
9. KADUDA - Huyu ndie Jogoo-fisi, kazi yake nikusubiri Admin kuongeza wanadada, hapo basi kazi yake kukaribisha wanadada wageni na nia za kifisi.
10. YOHANA - Hawa basi ndio wale wakuleta maombi na neno la Mungu kwenye grupu.
11. MABANDI - Kazi yao kuleta screeni shoti za fesibuku, twirra na ata instagram kwenye grupu.
Jee wewe mwenzangu ni yupi kati ya hao wenzetu?
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.