ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 7, 2015

MEYA MANISPAA YA KINONDONI AKABIDHI SOKO LA MAWASILIANO SIMU 2000

Meya wa manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akiwa na watendaji wa soko hilo wakikagua vizimba kabla ya kuwakabidhi wafanya biashara.
Na Mwandishi wetu

MSTAHIKI  Meya wa manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda  amesema kuwa soko jipya la SIMU 2000 litaweza kuchukua wafanyabiashara 512 kutoka kila pembe ya manispaa ya kinondoni.

Mwenda amewatoa hofu wafanyabiashara wa soko jipya la kituo cha basi cha Simu2000 mawasiliano  kuwa watafanya biashara bila ya kuwa na matatizo yoyote kwa kuwa soko hilo lipo katika mfumo wa kisasa.

Mwenda alisema hayo alipokuwa akikabidhi vizimba vya soko hilo kwa wafanya biashara ndondogo waishio katika wilaya ya kinondoni na sio mtu kutoka eneo la nje ya manispaa hiyo hivyo kuwataka kulitunza soko hilo kama mali yao.

“tumeamua kulifanya soko hili hili liweze kuanza kazi kabla ya uzinduzi rasmi utakaofanywa baadae hili kuweza  kuwapa fursa wafanya biashara kuliko kuacha jingo limeisha na kuonekana kama picha hivyo nawaomba mfanye biashara hili muweze kujiongeza kipato” alisema Mwenda.


Alitoa wito kwa wafanyabiashara hao kutokata tama kwani mwanzo ni mgumu kwnai eneo lenyewe ni jipya hivyo sio rahisi kuona biashara ikichanganya kwa haraka kama wanavyofikiri.


Meya wa Manispaa ya Kinondoni akiongea na wafanyabiashara wa soko la simu 2000 
Wakati huo huo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imesaini mkataba wa mashirikiano ya kusaidiana na jiji la Humburg ,mkataba huo umesainiwa leo na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda aliye ambatana na Mkurugenzi wake Eng.Mussa Natty, Utajengwa mtambo wa kuchakata taka za ugani na kuzalishwa mbolea Mabwepande wenye thamani ya shilingi za kitanzania ni bilioni 3.5 ambazo zitatolewa na jiji la Humburg .


Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mkataba huo Mstahiki Meya alisema ukishajengwa mtambo huu Kinondoni itakuwa umetatua tatizo la upatikanaji wa mbolea kwa wakulima nchini, pia mradi huo utatatuwa uhaba wa ajira kwani unamakadirio ya kutengeneza zaidi ya ajira 1000.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.