ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 17, 2015

KWETU HOUSE 2015 MSIMU WA PILI YATUA JIJINI MWANZA KUSAKA VIPAJI KWA MASHABIKI WA SOKA MSHINDI KULAMBA MILIONI 15

Team ya Kwetu House 2015 Msimu wa Pili wakiwa Studio za Jembe FM 93.7 Mwanza Mara Baada ya Mahojiano kuhusiana na KWETU HOUSE 2015 Kwa Jiji la Mwanza
Msimu wa pili wa Kwetu House  - “kwetu house, kipaji zaidi ya soka” hili shindano ambalo hujumuisha zaidi wapenzi wa soka wenye Kipaji,  jumla ya mikoa mitano (Arusha, Zanzibar, Dodoma, Mbeya na Mwanza) kutoa washiriki zaidi kwa ajili ya kunogesha na kuleta upinzani wa kutosha msimu huu mshindi ataondoka na kitita cha shilingi milioni 15, tofauti na msimu uliopita ambao ilikuwa Sh milioni 10.
Mkuu wa Channels Azam TV Madam Stellah Adam akizungumzia KWETU HOUSE 2015 kwa Mwaka huu ambapo Kauli mbiu ni "Kipaji na Soka" Stellah aliongezea Zawadi ya Mshindi wa Mwaka huu imeongezeka kutoka milioni 10 Msimu uliopita Hadi Milioni 15 Kwa Msimu huu wa Pili
Kwetu House 2015 Wakiwa Studio za Jembe FM 93.7 Mwanza Kuzungumzia Msimu wa Pii wa KWETU HOUSE 2015 kwa Jiji la Mwanza.

Baada ya Kwetu House  kusaka Shabiki mwenye Kipaji Kwenye Mikoa ya Arusha, Zanzibar,Dodoma na Mbeya sasa ni zamu ya ROCK CITY *Mwanza  kwa Mashabiki wote wa Soka wenye Vipaji tofauti (Mwimbaji,Mchekeshaji,mbunifu wa mavazi,mchoraji n.k) kuonyesha vipaji vyao na hatimye Kupata washiriki watakao iwakilisha Jiji la Mbeya kwenye Jumba la  (Kwetu House ) jumla ya washiriki 20 kutoka Mikoa Mitano kukaa kwenye Nyumba ya Kwetu House  

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.