ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 13, 2015

AIRTEL FURSA YAMWEZESHA KIJANA MFUGA KUKU

Mohamed Said (katikati)  akimwelekeza  Meneja huduma za jamii wa Airtel,  Hawa Bayumi (Kulia) baada ya kukabidhiwa banda la kuku la kisasa pamoja na kuku wa kienyeji kutoka Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel Fursa, wenye dhamira ya kuwawezesha vijana
Meneja huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (Kulia) akiongea na waandishi wa habari , baada ya kumkabidhi Mohamed Said (Kushoto) banda la kuku la kisasa pamoja na kuku wa kienyeji kutoka Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel Fursa, wenye dhamira ya kuwawezesha vijana.
Mohamed Said akiwalisha kuku baada ya kukabidhiwa banda la kuku la kisasa pamoja na kuku wa kienyeji kutoka Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel Fursa, wenye dhamira ya kuwawezesha vijana.
Meneja huduma za jamii wa Airtel,  Hawa Bayumi (Kulia) akimpongeza Mohamed Said (Kushoto) mara baada ya kumkabidhi banda la kuku la kisasa pamoja na kuku wa kienyeji kutoka  Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel Fursa, wenye dhamira ya kuwawezesha vijana.
Meneja huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (Kulia), Mohamed Said (wa pili kulia) na majirani (kushoto) wakikagua banda la kuku la kisasa pamoja na kuku wa kienyeji  alivyokabidhiwa  Mohamed kutoka Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel Fursa, wenye dhamira ya kuwawezesha vijana.

AIRTEL FURSA YAMWEZESHA KIJANA MFUGA KUKU
Vijana wengi wana ndoto za kujiletea maendeleo lakini wanashindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kukosa elimu sahihi na kutokuwa na mitaji ambayo ingewawezesha kujiunga kwenye miradi ya ujasiriamali.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa AIRTEL FURSA imeiona changamoto hiyo na kuamua kuwafikia vijana ambao wameonesha jitihada za kujikwamua na umaskini kwa kuwawezesha kupata mitaji ama vifaa vitakavyotimiza ndoto hizo.

Mohmed Saidi Kigumi  Kijana Mfugaji wa kuku wa kienyeji mwenye umri wa miaka 24 aishie  Kiluvya nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam amekataa kusubiri kuajiriwa na amethubutu na kuanzisha mradi huku akitoa wito kwa vijana kujitokeza kukabiliana na changamoto zinazokwamisha kujiletea maendeleo.

“Nawashukuru sana Airtel kwani wameweza kubadilisha maisha yangu.

Nilianza na kipato kidogo sana nikiwa na kuku watatu katika banda lakini kwa juhudi zangu na msaada mkubwa kutoka Airtel leo hii nimeweza kuwa na kuku zaidi ya 150, banda la kisasa ili kufanya ufugaji wa kisasa na tank kubwa la maji ili kuweza kuhudumia kuku wake kwa urahisi.Si hivyo tu Airtel imeniwezesha kupata mafunzo ya kuendesha biashaya yangu, kutunza mahesabu na mambo mengine mengi yatakayonifanya niwe imara kibiashara.

Aliongeza kwa kusema, “moja na moja huzaa mbili, Ndoto zangu ni kulifikia soko la Afrika Mashariki, Niweze  kuwa mfanyabiashara mkubwa na kuweza kusambaza kuku wangu kwenye masupamaketi makubwa nchini na hata nje ya nchi. Hii itanisaidia kuniinua kiuchumi mimi na familia yangu na hata uchumi wa nchi yetu”.

Akizungumza baada ya makabidhiano, Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi alisema Kwa Airtel kudhamini juhudi za Mohamed ambaye anajiingizia shilingi 50,000 kila siku kwa kuuza mayai ya kuku wa Kienyeji,  kadhalika tumewawezeesha vijana zaidi ya 500 kupata semina za mafunzo ya ujasiriamali zilizofanyika katika mikoa ya Dar es Saalam na Mwanza.

“Mohamed ni kijana wa nne kufaidika na mpango huu na kama tulivyosema hapo awali mpango huu unawalenga vijana ambao tayari wanajihusisha na miradi mbalimbali kama Mohamed na wanatakiwa kutuma maombi yao.”

alisema na kusisitiza kuwa mpango huo hauwalengi wanaotaka kuanzisha miradi bali ambao tayari yameshaanzisha biashara zao na wanahitaji kuwezeshwa.

Alimtaka Mohamed atumie vizuri mafunzo aliyopatiwa katika semina aliyopewa kabla ya kukabidhiwa banda na vifaa hivyo vizuri iliaweze kujiendeleza zaidi na kuwa mfano mzuri kwa vijana ili kujiinua kimaisha yeye na familia yake.

“Ili kijana kushiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com> ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara.

Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtelwww.airteltanzania.com>

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.