ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, June 14, 2015

TUZO ZA KILI 2015 KATIKA PICHA

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda(kulia) akimkabidhi ndugu wa karibu wa Mwanamuziki, Ally Kiba Tuzo ya tano katika hafla ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 USIKU WA TUZO ZA KILLIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS 2015. 
 Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza(kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka kwa niaba ya aliyekuwa Mkurugenzi wa TOT, Marehemu Kaptani John Komba Tuzo ya udau wa Muziki aliyefanikisha maendeleo ya Muziki (Hall of Fame).
 Mwakilisji wa Yamoto Bendi akitoa shukrani mara baada ya Bedi hiyo kutwaa Tuzo ya Kikundi bora cha Mwaka-Bongo Fleva.
 Mkurugenzi wa Jahazo Modern Taarabu, Mzee Yusuf akitoa shukrani mara baada ya kutwaa tuzo ya Kikundi bora cha mwaka -TAARAB.
 Mwanamuziki wa FM Academi, Nyoshi akitoa shukrani mara baada ya bendi kutwaa tuzo ya Bendi bora ya Mwaka.
 Mwanamuziki wa nyimbo za kizazi kipya, Mwana FA akitoa shukrani mara baada ya kutwaa Tuzo ya Wimbo bora wa kushirikishwa /kushirikiana.
 Mwanamuziki Chipukizi, Baraka Dra Prince akitoa shukrani  mara baada ya kutwaa Tuzo ya Usanii bora Chipukizi anayeibukia.
 Burudani kutoka Ommy Dimpos wakati wa tuzo hizo.
 Msanii wa nyimbo za Mashahiri, Mrisho Mpoto akionyesha tuzo yake aliyotwaa katika kapengele cha Wimbo bora wenye vionjo vya asili ya Kitanzania.Wimbo wake wa Waite waite ndio ulishinda. 
 Ndugu wa karibu wa Mwanamuziki, Diamond Platinum,akitoa shukrani mara baada ya Diamond kupata tuzo kwanza ya Wimbo bora wa Zouk/Rhumba.Wimbo wa Nitampata wapi ndio ulishinda.
 Ndugu wa Ally Kiba wakitoa shukrani mara baada ya mwanamuziki huyo kupata Tuzo ya kwanza ya Wimbo bora wa Afro Pop.
 Ndugu wa karibu wa msanii wa Diamond Platinum akishukuru mara baada ya msanii huyo kupata Tuzo ya pili ya Video Bora ya Mwaka, ambapo wimbo wa Mdogo mdogo kushinda.
 Mwanamuziki, Barnabas akitoa burudani wakati wa hafla hiyo
 Mwanamuziki, Vanesa Mdee akitoa burudani wakati wa hafla hiyo.
 Mtayarishaji (producer) bora wa nyimbo ya mwaka ya Bendi, akitoa shukrani, Amoriso. 
 Ndugu wa karibu wa Kampuni ya Enrico wakitoa shukrani mara baada ya kutwaa Tuzo ya Utayarishaji bora wa nyimbo ya Taarabu. 
 Hanreel akitoa shukrani mara baada ya kutwaa Tuzo ya utayarishaji bora wa nyimboya Mwaka ya Bongo fleva.
 Msanii wa nyimbo za kizazi kipya, Joh Makini akitoa shukrani mara baada ya kupata Tuzo ya utunzi bora wa mwaka wa Hip Hop.

 Msanii, Ben Paul akitoa burudani wakati wa hafla hiyo
 Mwimbaji Ben Paul akitumbuiza nyimbo yake ya Sofia Sofia.
 Mwimbaji, Jose Mala akitoa shukrani mara baada ya kutwaa tuzo ya utunzi bora wa mwaka wa bendi.
 Ndugu wa Msanii, Ally Kiba wakipokea tuzo ya pili ya utunzi bora wa mwaka wa utunzi bora wa nyimbo ya bongo fleva kutoka kwa Maria Saringi.
 Mkurugenzi wa JAHAZI Morden Taarabu akipata tuzo nyingine ya wimbo bora wa mwaka wa Taarabu kutoka kwa Masudi Masudi. 
 Raia wa Kikenya akipokea tuzo kwa niaba ya wimbo bora wa mwakawa  Afrika Mashariki,Ibrahim Sameer.
 Burudani timukutoka kwa Malaika BENDI

 Mwanamuziki, Joh Makini akitoa shukrani mara baada ya kupata tuzo nyingine tena ya Msanii Bora wa Hip Hop.
 Rapa, Saulo Ferguson akitoa shukrani mara baada ya kupata Tuzo ya Rapa bora wa  mwaka wa  Bendi.Kulia ni Mke wake.
 Rapa , Saulo FERGUSO akirapu mara baada ya kunukiwa tuzo.
 Msanii wa chipukizi, Maua Sama akitoa shukrani mara baada ya kutwaa tuzo ya mwaka ya  wimbo bora wa reggae/Dance Hall
 Mwanamuziki Profesa J, akitoa shukrani mara baada ya kutwaa tuzo ya wimbo bora wa mwaka wa HIP HOP.
 Muimbaji, Jux akitoa shukrani mara baada ya kutwaa tuzo ya mwaka ya Kill ya nyimbo ya wimbo bora wa R&B. 
 Meneja uzamini, George Kavishe akimkabidhi tuzo, mwakilishi wa bendi ya Fm academia mara baada ya kutwaa tuzo ya wimbo bora wa Kiswahili wa Bendi. 
 Ashukuru kwa mashabiki na wapenzi
 Ndugu wa karibu wa Muimbaji, Ally Kiba wakitoa shukrani mara baada ya ndugu yao kutwaa tuzo ya tatu ya Wimbo bora wa MWAKA 2015.
 Mishi Bomba(kushoto) akimkabizi Isha Mashauzi tuzo mara baada yakutangazwa mshindi wa wimbo bora wa mwaka wa Taarabu.
 Wasaii WEUSI wakitumbuiza jukwaani wakati wa hafla ya tuzo hizo.

 Muimbaji, Jose Mara akitoa shukrani mara baada ya kupata tuzo ya uimbaji bora wa mwaka wa kiume - Bendi.
 Isha Mashauzi akitoa shukrani mara baada ya kutwaa tena Tuzo ya Mwimbaji bora wa mwaka wa kike wa Taarabu.
 Mzee Yusuf akipokea tuzo nyingine kutoka kwa Dr. Mwakalinga-COSOTA, ya muimbaji bora wa muimbaji bora wa Mwaka wa Taarabu.
 Vanesa Mdee akitoa Shukrani mara baada ya kutunukiwa tuzo ya Mwaka ya Muimbaji bora wa Mwaka wa kike wa Bongo Fleva.
 Ndugu wa Ally Kiba wakipokea tuzo ya nne ya mwimbaji bora wa kiume wa Bongo Fleva kutoka kwa Sudi Brown
 Muimbaji Vaneza Mdee akifurahi na wacheza shoo wake mara baada ya kutunukiwa tuzo ya pili ya Mtumbuizaji bora wa mwaka wa kike.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.