Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali ya
habari mkoani Kilimanjaro.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya
Jamii Kanda ya Kaskazini.
SIKU moja
baada ya kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kumlipua mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas
Gama kwa madai ya kufanya udalali na ufisadi katika uporaji wa ardhi ya wananchi ,mkuu
huyo amejitokeza
mbele ya wanahabari na kukanusha tuhuma
hizo.
Katika utetezi wake Gama alirejea kauli yake
aliyoitoa miaka sita iliyopita ya kuwa
yeye ni msafi huku akiitupia mzigo halmashauri ya wilaya ya Rombo tuhuma za kiasi cha sh Mil 500
zilizotajwa kutolewa wawekezaji wa
Kichina kama fidia kwa wananchi katika ardhi
kilipojengwa
kiwanda cha kutengeneza Saruji.
Alisema tuhuma
zilizotolewa Bungeni dhidi yake si za kweli na
kwamba ni za kisiasa huku akitaja
sababu ya kuibuliwa kwa tuhuma hizo kuwa ni kutokana na juhudi zake za kupambana na Pombe
haramu katika wilaya ya Rombo
pamoja na Urejeshwaji wa wafanyabiashara katika soko la kati
la mjini Moshi.
“Nataka niwaambie hii ni siasa,zipo issue nyingi
zilizochangia kuibuka kwa haya
mambo ,lakini nawaambieni mbili tu,Issue ya kwanza
Pombe Rombo,na msimamo wangu juu ya
Pombe Rombo ndio imeza hii,la pili ni
soko la Moshi
mjini,watu wana agenda zao kwenye soko hilo
,wananchi wamerudi pale
,imewaumiza watu.”alisema Gama.
“Watu walitaka
Pombe ya Gongo iharalishwe,mimi nimesema hadharani anayetaka pombe ya Gongo ihararishwe si mwenzetu
mu mshughulikie kwa maana si mwenzetu
sasa hili limeleta nongwa”aliongeza Gama.
Akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma hizo ,Gama amekiri
mtoto wake aliyetajwa kwa
jina la Mayunga Leonidas Gama kuhusika katika uanzishaji wa kiwanda hicho huku akihakikisha
kiwanda hicho kinajengwa katika mkoa
wa Kilimanjaro badala ya Bagamoyo kama walivyo pendelea
wawekezaji
hao.
“Kiwanda cha saruji kinachojengwa pale Rombo,
nilikuwa na uwezo wa kukipeleka popote
ninapotaka mimi, lakini mimi binafsi ndiye niliyefanya juhudi kiwanda kile kijengwe
Kilimanjaro, mimi binafsi na wala sio mtu mwengine, nimefanya juhudi hizo kwa
lengo la kuongeza
ajira kwa wananchi na kuinua uchumi wa mkoa huu”,
alisema Gama .
“Historia ya Kiwanda hiki iko wazi, na
nililipeleka hadi kwenye kikao cha ushauri wa mkoa (RCC),nanaomba nieleweke
kwamba, ni juhudi zangu na za mtoto
wangu, nilitamka kwenye kikao kile na wala
sikuficha, mtoto wangu ambaye
ametajwa yeye ana rafiki yake wa kichina, wala si
kweli kwamba hii
kampuni mimi nimekwenda kuichukua China kwa gharama za serikali” aliongeza Gama.
Alisema katika kikao hicho (RCC), Mbunge wa Rombo,
Joseph Selasini, Mbunge wa Vunjo,
Dkt. Augustino Mrema na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, walishiriki katika kikao
hicho na kwamba baada ya mvutano
ndipo makubaliano yakawa kiwanda kijengwe wilaya ya Rombo .
“Toka siku ile mimi kama mkuu wa mkoa nikakabidhi
madaraka wilaya ya Rombo, kwa hiyo
shughuli zote za ujenzi ,shughli zote za kutafuta viwanja ziifanywa na halmashauri ya wilaya ya
Rombo na sio Gama”alisema
Gama.
Alisema waliolipa fidia na kununua viwanja ni
halmashauri ya wilaya na hata eneo
kilipojengwa kiwanda hicho ni mali ya halmashauri ya
wilaya ya Rombo na si cha mwekezaji
kama inavyoelezwa .
“Nimeelezwa kweye
tuhuma kuwa nimepewa milioni 500,hii ni hadithi ya kisiasa ,sijapokea kiasi hicho cha fedha wala
sikijui,hata hizo hisa 20,000
nilizoambiwa ninazo kwa kweli sina ,kama ningekuwa nazo ni
haki yangu kwa sabau sijavunja
sharia lakini sin ahata hisa moja.”alisema
Gama.
“Swala mtoto wangu kuwa na hisa si dhambi na ni
haki yake kisheria,kwa
sababu yeye ndiye aliyewatafuta hao watu na ni
rafiki zake ,wala si
mimi niliyewaleta kama amenunua hisa huko ni hiari
yake,mimi sina hisa
kama Gama,sijapokea milioni 500 kama gama,mimi si
dalali na kama ni
udalali wa ardhi hiyo itakuwa ni halmashauri ya
wilaya ya Rombo na si
gama.”alisema Gama.
Alipoulizwa endapo kama halmashauri ya wilaya ya
Rombo itakuwa inamiliki sehemu
ya hisa katika kampuni hiyo kutokana na utolewaji wa ardhi yake ,Gama alisema wenye majibu ni
halmashauri ndio watakuwa wanajua ni
mikataba gani wameingia na wawekezaji hao.
Kuhusu eneo la Uwekezaji wa soko la Lokolova, Gama
alisema ameshangazwa na kauli za kuwa
yeye ni fisadi wa ardhi katika eneo hilo wakati makubaliano ya kuanzishwa kwa soko la
kimataifa na ji mdogo wa kibiashara
ulipitishwa katika kikao cha RCC ambacho pia Mbunge
wa Vunjo, Dkt. Augustino Mrema
alihudhuria na kusifia mpango huo.
Sakata la Kiwanja
cha Mawenzi, Gama alisema yeye kama mkuu wa Mkoa, alichokifaya ni kuishauri Halmashauri ya Manispaa
ya Moshi kufuata Sheria za
umilikishwaji wa Ardhi ili kuepusha Halmashauri
kufilisiwa kwa kukiuka
taratibu.
Juzi wakati akiwasilisha bungeni maoni ya kambi
rasmi ya upinzani kuhusu bajeti yay
a wizara ya ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi kwa mwaka wa fedha 2015/2016,msemaji mkuu wa kambi
hiyo Halima Mdee
alimrushia tuhuma Gama za kuhusika katika kutumia
fedha za serikali kwenda nchini
China kutafuta watu wawili wanaotajwa kama wawekezaji.
Katika taarifa hiyo Mdee alidai katika hali isiyo
ya kawaida nay a kushangaza watu
hao katika ardhi iliyokwisa lipiwa fidia kwa fedha
za umma ,ilianzishwa kampuni
binafsi ya Jun Tu Investment International Company Ltd.
|
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.