DC Makonda akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wakati alipo watembelea waathiriwa hao. |
Wananchi wakiwa katika maeneo hayo yaliyoathiriwa na mmomonyoko huo. |
Baadhi ya nyumba zilizobomoka kutokana na mmomonyoko huo. |
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amepiga marufuku uchimbaji mchanga katika mto Mbezi na Kawe Ukwamani kutokana na uharibifu wa mazingira ambao umesababisha nyumba zilizo kando ya mto huo kubomoka kutokana na mmomonyoko wa ardhi.
Makonda alipiga marufuku wakati akizungumza na wananchi walioathiriwa na mmomonyoko huo alipofika kuwapa pole na kuona jinsi ya kuwasaidia Dar es Salaam jana.
"Wakati tunaangalia namna ya kuwasaidi naomba kuanzisha leo shughuli za uchimbaji wa mchanga katika mto Mbezi ukome na mtu atakaye bainika anaendelea kuchimba mchanga atachukuliwa hatua za kisheria" alisema DC Makonda.
Makonda alisema wataalamu wa Manispaa hiyo watafika katika eneo hilo ili kuona nini kifanyike kupunguza tatizo hilo kwa siku za mbele kama walivyofanya maeneo ya Tegeta yaliyokumbwa na mafuriko ambapo kutajengwa karavati kubwa ili maji yaweze kupita.
Katika eneo hilo nyumba zaidi ya 100 zimebomoka kutokana na kusombwa na maji wakati wa mvua za maisha huku zikiwaacha wakazi wa maeneo hayo wakiishi katika chumba kimoja na wengine wakikosa makazi. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.