Kocha Mkuu mpya wa timu ya Coastal Union,Jackson Mayanja kushoto akisaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu hiyo kulia ni Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi, |
Na Mwandishi Wetu, Tanga
MABINGWA
wa Ligi kuu soka Tanzania bara mwaka 1988, Coastal Union, Wagosi wa Kaya
imeingia mkataba wa miaka miwili na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Jackson Mayanja ambaye ni raia wa
Uganda kuifundisha timu ya Coastal Union katika msimu ujao wa Ligi kuu
soka Tanzania Bara itakayoanza Mwezi Agosti mwaka huu .
Utiliaji
wa saini wa Kocha huyo ulifanyika (leo)jana mjini hapa na kuhudhuriwa
na viongozi mbalimbali wa timu ya Coastal Union akiwemo Mjumbe wa Kamati
ya Utendaji Albert Peter na Katibu Mkuu wa timu hiyo,Kassim El Siagi.
Akizungumza
baada ya kumalizika zoezi hilo,Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar
Assenga amesema kuwa kutokana na umahiri aliokuwa nao kocha huyo
wanaimani kubwa ataipa mafanikio timu hiyo hasa katika harakati za
kuhakikisha inafanya vizuri ligi kuu msimu ujao.
Amesema
kuwa uwezo wa Kocha huyo utaleta matumaini makubwa ya mafanikio hasa
ukizingatia ni kocha mwenye uwezo mzuri wa kufundisha na kuzipa
mafanikio timu hivyo tunaamini kuja wake kwetu itakuwa chachu katika
maendeleo.
Mayanja
ambaye aliwahi kuzifundisha timu za soka Kiyuvu FC ya Rwanda,Timu ya
Mamlaka ya Mapato nchini Uganda (URA),Vipers FC ya Bunamwaya na KCC ya
Uganda amesema kutua kwenye timu hiyo kumpa faraja kubwa hivyo
atahakikisha anatoa mchango wake kwenye kuipa mafanikio.
Amesema
kuwa mipango yake mikubwa ni kuhakikisha timu hiyo inang’ara katika
michuano ya Ligi kuu msimu ujao ikiwemo kubadili aina ya mchezo wa timu
hiyo ili iweze kupata mafanikio kwa kuweka umoja baina ya wachezaji
mashabiki, wanachama na wapenzi.
Amesistiza
pia umuhimu wa mshikamano baina ya wapenzi,wanachama na viongozi ili
kuiwezesha timu hiyo kuchukua Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao kwani
dhamira yake ni kutaka kuona timu hiyo inang’ara kwenye medani za
kitaifa na kimataifa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.