ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 30, 2015

EWURA YAFUNGUA OFISI MPYA MWANZA

MKUU wa wilaya ya Nyamagana mkoani |Mwanza Baraka Konisaga amesema kuwa kufunguliwa kwa ofisi za EWURA Kanda ya ziwa kutasaidia kukabiliana na changamoto zilizokuwepo katika utendaji na udhibiti kwa wakati.
Jiwe la msingi limewekwa.
Ofisi za EWURA.
Mkurugenzi wa EWURA Ndug. Felix Ngamlagos.
 AIDHA Mkurugenzi wa EWURA Ndug. Felix Ngamlagos amesema kuwa kwa hivi sasa matumizi ya mafuta yameongezeka nayo serikali inahitaji kunufaika kupitia matozo mbalimbali ya kodi toka kwa wachuuzi hivyo amewaomba wananchi wanunuapo mafuta kuhakikisha kuwa wanachukuwa risiti ili kusaidia kukuza uchumi.

Amezitaja pia moja kati ya faida za kuchukuwa risiti pindi yafanyikapo manunuzi ni kuwa na uthibitisho au kitambulisho pindi mwananchi anapogundua kuwa amenunua mafuta yasiyo na viwango au yaliyochakachuliwa ambayo yameleta madhara kwenye chombo chake cha usafiri au chombo chochote cha nishati.












PICHA ZOTE NA ZEPHA WA GSENGOBLOGSPOT

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.