Wafanyakazi wa Airtel wakishusha zawadi zilizokabidhiwa kwa Bertha Benedict (hayupo pichani) mkazi wa Bunju Jijini Dar es Salaam baada ya kuwezeshwa na mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha”. |
Airtel FURSA yawawezesha vijana wajasiriamali Dar
KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel Fursa ambao umelenga kuwawezesha vijana wajasiliamali wadogo wadogo nchini umetoa msaada mwingine tena jijini Dar es salaam kwa msichana mjasiriamali Bertha Benedicto.
Bertha ambaye amelelewa katika Kituo cha Kulea watoto cha Dogodogo Center Kilichopo Bunju Jijini Dar es Salaam na kuhitimu mafunzo ya mwaka mmoja ya ufundi wa kushona nguo kituoni hapo amepatiwa vifaa mbalimbali pamoja na cherehani ya kisasa ili kuendeleza ujuzi wake.
Akiongea wakati wa makabithiano Meneja wa mahusiano ya jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi alisema “ Airtel tumeona ni vyema kupitia mpango wetu wa Airtel Fursa kumpatia vifaa na mashine hii ya kisasa ya kushonea Bi Bertha Benedecto kwa lengo la kumwezesha kuendesha shughuli zake za kiuchumi kwa ufanisi zaidi. Sambamba na hilo tumeweza kumpeleka kwenye mafunzo ya kumsaidia kujijenga, kuweka mahesabu yake na kuendesha biashara yake ili aweze kukuza biashara na kuisaidia familia yake”.
Tunaamini hii ni nafasi ya pekee kwa vijana wadogo kati ya umri wa miaka 17 mpaka 24 walioko katika maeneo mbalimbali ya nchi kuweza kufaidika na mpango huu wa Airtel Fursa wenye lengo la kuwawezesha vijana wajasiriamali wadogo wadogo kukuza mitaji na biashara zao kwa ujumla. Aliongeza Bayumi”
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Bertha amesema vifaa hivyo vitamwezesha kuendesha maisha yake na familia kwa ujumla huku Mama yake Immaculate Makinda akiishukuru Airtel kwa kuwa mkombozi kwao.
Bertha alisema, “nawashukuru sana Airtel kwa kuweza kufanikisha ndoto zangu. Kwa kuweza kunipatia vifaa hivi vya kisasa. Nimekuwa nikipata ugumu wa kupata wateja kwani sikuwa na vitendea kazi vya kutosha vitakavyoweza kukidhi mahitaji ya wateja wangu lakini sasa naamini nitapata wateja wengi sana na kuinua biashara yangu”
Kwa upande wake Mratibu wa Dogodogo Centre, bw.Issa Buzohela alisema, anaiomba kampuni ya Simu ya Airtel kuendelea kukisaidia kituo hicho na kuinua vipaji vya vijana kwani nchi yetu imezungukwa na vijana wenye vipaji mbalimbali lakini hawana uwezo wa kuendeleza vipaji vyao.
Mpaka sasa Airtel Fursa imeshawawezesha vijana mbalimbali na kuboresha shughuli zao za kiuchumi kwa kuwapatia vitendea kazi na kuwaingiza katika warsha za mfunzo ya Airtel Fursa ili waweze kutimiza ndoto zao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.