ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 1, 2015

RAIS Dkt. KIKWETE "NISINGEKUWA RAIS NINGEKUWA MSANII MKALI WA BONGO FLEVA"

























 RAIS Dkt. Jakaya Kikwete, ametamba kuwa angekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya basi angelikuwa wa “BongoFleva” kutokana na kuwa na sauti nzuri yenye kumudu kuimba nyimbo kwa ufasaha zaidi.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Mwanza kwenye uwanja wa michezo wa CCM Kirumba wakati wa maadhimisho ya kilele cha sherehe za Mei mosi zilizofanyika Kitaifa jijini Mwanza kwa mwaka huu wa mwisho wa utawala wake.

Dkt. Kikwete akiimba wimbo wa Bendi ya OSS (Ochestra Safari Sound) wenye mashairi yasemayo "mimi msafiri bado niko njiani sijui lini nitafika... naulizia watu kule ninakokwenda....”  na kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa dansi waliomshangilia ambapo alijigamba kuwa na sauti ya mauzo.

“Mmesikia sauti yangu si mbaya sana,  hakika nisingekuwa Rais wa Nchi hii basi nigekuwa msanii wa bongo fleva kama akina Ali Kiba, Diamond na wasanii wengine wakali nikiuza album zangu kwani ninge kuwa tishio kwa kuimba lakini sikujaliwa kuwa masanii lakini najua kwa kiasi flani kuziimba nyimbo za baadhi ya bendi zilizokuwa maarufu hapa nchini,” alisema.

Rais pia alimpongeza msanii maarufu nchini wa kizazi kipya mwenye mashairi na misamiati ya maneno magumu, Mrisho Mpoto, kwa kumtaka kujibu bango la walimu lililokuwa na ujumbe uliosomeka “Shemeji Unatuachaje??” ambapo alijibu kwa kusema kuwa kuoa mwalimu nitabu kweli kweli haya nimesikia.

Aliwapongeza viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) nchini kwa kumwalika Mpoto “Mjomba” mara nyingi amekuwa akitoa ujumbe mzito kupitia fani yake ya muziki na mashairi lakini yakifikisha ujumbe bara bara kwa wananchi katika sherehe mbalimbali za kitaifa na makongamano .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.