ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 18, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONYESHO YA BIASHARA NCHINI CHINA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Kamati ya maandalizi ya Maonyesho ya Biashara ya China 'Expo Central China 2015', wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa 'Wuhan International Exhibition Centre VVIP Room'. Mkutano huo umeanza leo Mei 18 2015 jijini Wuhan, Jiombo la Hubei. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akiwa na baadhi ya Viongozi wa nchini China, Katibu  wa Chama Tawala cha CPC cha Nchini China, Jimbo la Hubei, Li Hongzhong (kushoto) na wengine, wakati alipofungua Maonesho ya Biashara ya China  'Expo Central China 2015', yaliyoanza leo Mei 18, 2015, Jimbo la Hubei, Jijini Wuhan nchini China. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Maonesho ya Biashara ya China, 'Expo Central China 2015', ulioanza leo Mei 19, 2015 kwenye ukumbi wa mikutano wa 'Wuhan International Exhibition Centre, uliopo Jijini Wuhan Jimbo la Hubei nchini China. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa China, Wang Yang, wakati walipokutana kwa mazungumzo baada ya Makamu kufungua rasmi Maonesho ya  Biashara ya China, leo Mei 18, 2015 kwenye Ukumbi Mikutano wa 'Wuhan International Exhibition Centre, jijini Wuhan Jimbo la Hubei nchini China. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza wa na  Katibu  wa Chama Tawala cha CPC cha Nchini China, Jimbo la Hubei, Li Hongzhong, baada ya kuzungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na  Katibu  wa Chama Tawala cha CPC cha Nchini China, Jimbo la Hubei, Li Hongzhong (kushoto)  wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara ya China  'Expo Central China 2015'. Picha na OMR
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
 MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AHUTUBIA MAONESHO YA NANE YA BIASHARA JIJINI WUHAN JIMBO LA TUBEI, NCHINI CHINA 

Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo Jumatatu Mei 18, 2015 amehutubia katika maonesho ya Biashara kwa Ukanda wa Kati wa China, Maonesho yaliyofanyika katika mji wa Wuhan akiwa mgeni Mwalikwa. 

Maonesho haya yanajumuisha miji mbalimbali ya ukanda wa Kati wa China nayanalenga kuunganisha fursa za Biashara na Uwekezaji ndani ya China na nje ya nchi hiyo.

Katika Hotuba yake ya ufunguzi wa Maonesho hayo, Naibu Waziri Mkuu wa China Wang Yang aliwaeleza mamia ya waliohudhuria shereheza ufunguzi wa maonesho hayo kuwa, China inafungua fursa mpya na inahitaji kuona maeneo yote ya nchi yanakuwa na maendeleo ya nayokaribiana na akaongeza kuwa, fursa za biashara na uwekezaji zipopia katika nchi zingine hasa Bara la Afrika ambalo ni Bara lenye urafiki na ukaribu na China kwa muda mrefu. 

Naibu Waziri Mkuu huyo aliongeza kuwa, amefurahi kuona nchi kadhaa zimewakilishwa katika maonesho hayo na akaelkeza kuwa uwepo wamgeni Mwalikwa yaani Dkt. Bilal kunaonesha udhati ilionao China kuhusu mahusiano yake na Afrika na akawataka wawekezaji waliohudhuria sherehe hizo kutambua kuwa mahusiano ya China na Afrika yatakuwa yenye manufaa pale watakapo tumia fursa za uwezo wao katika mitaji kuwekeza katika Afrika kwani mazingira ya bara hilo ni rafiki kwa China.

Katika hotuba yake kama Mgeni Mwalikwa, Makamu wa Rais Dkt. Bilal alifafanua kuwa, China imekuwa rafiki wakaribu na ndugu kwa nchi mbalimbali za Afrika hivyo basi, kuna kilasababu kwa China kuendelea kuwekeza katika Afrika hasa katika viwanda kwa kuwa kufanya hivyo situ kwamba kutanyanyua uchumi wa pande zote mbili, bali pia kutaongeza mahusiano ya nchi za Afrika na China.

 Kupitia mpango wake wakuendeleza viwanda Barani Afrika, China imepitisha nchi za Kenya Ethiopia na Tanzania kuwa za mfano barani Afrika na kwasababu hiyo, Mheshimiwa Makamu wa Rais aliwataka wawekezaji kutoka China kuja Tanzania kwa kuwa zipo fursa ambazo hazijatumika na kwamba hali ya kimaisha baina ya China na Afrika yanakaribiana hivyo ni rahisi kwa wekezaji wanaotoka China kuwekeza Afrika. 

Pia zlizungumzia uhusiano wa Tanzania na nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kuwa ni sababu nyingine ya Kijiografia inayosababisha Tanzania kuwa eneo bora kabisa kuwekeza kwa sasa kulinganisha na nchi nyingine za Ukanda huu wa Afrika.

 Katika hatua nyingine Mheshimiwa Makamu wa Rais alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu Wang Yang, ambapo katika mazungumzo hayo Mheshimiwa Makamu wa Rais alizungumzia uhusiano baina ya nchi zetu mbili na hasa mradi wa Bandari ya Bagamoyo sambamba na fursa zake punde utakapokamilika. 

Pia alizungumzia umuhimu wa China kutazama na mnayakuisaidia Tanzania katika utanuaji wa matumizi ya mkongo wa mawasiliano na eneo zima yaTeknolojia ya Habari na Mawasiliano, huku pia akigusia mradi wa ujenzi wa Uwanja wa ndege Zanzibar, mradi ambao umekuwa ukikabiliwa na vikwazo kadhaa na akasisitiza kuwa ni wakati vikwazo hivyo viishe na muda wa kuukamilisha ujenzi ufikie.

Katika mazungumzo yake pia alizungumzia suala la Reliya TAZARA ambapo alieleza kuwepo umuhimu wa pande zote tatu zinazohusika katika reli hii kukaa na kutafuta namna ya kuiimarisha iliiweze kuendana na changamoto za sasa kuliko ilivyo sasa. 

 Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu Wang wakati akijibu hoja za Mheshimiwa Makamu wa Rais alifafanua kuwa, China inaowataalam wenye uwezo wa kufanya tathimini ya fidia kwa wakaazi na hivyo inawezeka na nchi zetu kukubaliana kuwatumia ilikujua namna ya kukabiliana na suala la fidia kwa wakazi hasa wa Bagamoyo ili waweze kuachia eneo hilo litumike kwa ujenzi wa Bandari.

Pia alifafanua kuwa China inapenda kuona nchi za Tanzania, Zambia na China zinakaa meza moja ya mazungumzo ilikujadili kwa kina namna ya uendelezaji wa Reli ya TAZARA na kwamba mazungumzo hayo ya kifanyika nidhahiri kuwa Reli hiyo itakuwa ya manufaa kwa miaka mingine mingi ijayo.

Mheshimiwa Makamu wa Rais yupo nchini China kwa ziara maalum ya kikazi ambapo ataikamilisha kesho kutwa kwa kukutana na Makamu wa Rais wa China ambaye ndiye Mwenyeji wake katika ziara hii.

Makamu wa Rais pia ameambatana na Waziri wa Mawasiliano Sayansi naTeknolojia, Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah Kigoda na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali kutoka Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna. 

Mwingine ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.