ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 13, 2015

SOCCER CITY MABINGWA SAFARI NYAMA CHOMA 2015 JIJINI DAR ES SALAAM

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa (kushoto) na Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Gerald Ngiichi wakimkabidhi kikombe mchomanyama mkuu wa Bar Soccer City ya Sinza, Said Dando mara baada ya kuibuka mabingwa katika ma shindano ya Safari Lager Nyama Choma jijini Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Leaders mwishoni mwa wiki.
Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Gerald Ngiichi (wapilikushoto) wakimkabidhi kitita cha Shilingi 1,000 000/= mchomanyama mkuu wa Bar Soccer City yaSinza, Said Dando mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya Safari Lager Nyama Choma jijini Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Leaders mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa

Soccer City Mabingwa Safari Nyama Choma 2015 jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu.
SOCCER City Bar yenye makazi yake Sinza jijini Dar es Salaam wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager Nyama Choma 2015 yaliyofanyiaka mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Leaders Klabu na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi milioni moja na Kikombe.

Nafasi ya pili ilichukuliwa Chamanzi Bar ya Mbagala ambayo ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 800,000/=, nafasi ya tatu ni Liquid Bar ya Chang’ombe ambayo ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/=, nafasi ya nne ni High Way Bar ya Boko ambayo ilizawadiwa Shilingi 400,000/=, nafasi ya tano ni Amaholo  Bar ya Salasala ambayo ilizawadiwa Shingi 200,000/- na nafasi ya sita ni Kilwa road Bar ambayo ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 100,000/=

Akizungumza na wakazi jijini Dar es Salaam walifika katika mashindano hayo, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Gerald Ngiichi, kwanza aliwashukuru kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kwa kuendea kudhamini mashindano ya Nyama Choma ambapo kwa mwaka huu ni mara ya nane mfululizo kwani yamekuwa yenye mvuto wa pekee ambayo yanawapa picha halisi wakazi wa Dar es Salaam kuwa wapi wanaweza kupata nyama choma bora kutoka katika baa sita ambazo zimeingia fainali katika mkoa wetu.

Alisema Ngiichi kwanza kabisa tunawapongeza kwa kutoa elimu kwa wapishi wa baa mbalimbali ambayo mliaanza nayo hapo awali tunaamini kwa kupitia hilo wapishi wetu wameelimika sikama mlivyo wakutana hilo tuna washukuru na tunawaomba muendelee nalo kwani mnaongeza ajira kwa jamii kama sikupunguza umasikini.

Pili aliwapongeza baa sita zilizoingia fainali kwani wao ndio baa bora katika baa zote zinazo choma nyama mkoani humo na aliwaomba waendelee kuilinda hadhi na sifa hiyo waliyopewa na mwisho aliwapongeza mabingwa wapya Soccer City Bar kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2015 na kuwaomba ambao hawakufanikiwa kupata nafasi hiyo wajiandae kwa mashndano yajayo ya Safari Nyama Choma 2016.

Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa aliwapongeza mabingwa wa mwaka 2015, Soccer City na pia aliwashukuru wote walioshiriki toka mchakato ulipoanza mpaka kufikia kumpata bingwa lakini pia aliwashukuru wakazi wa jijini Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kuja kushuhudia nani anatwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma 2015.

Mwisho Edith aliwaomba washiriki wote ambao waliopata zawadi wakatumie vyema zawadi walizopata kwa kuboresha majiko yao kwa mashindano yajayo ya 2016 lakini pia wakawe mabalozi wazuri wa bia ya Safari Lager kwenye biashara zao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.