ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 10, 2015

SKYLIGHT BAND YAZIDI KUPASUA ANGA NA MUZIKI WA LIVE, NJOO USHUHUDIE LEO THAI VILLAGE

DSC_0616
Ni mwendo wa Nigerian Flava ni noma sana karibu leo ujione mwenyewe usisubirie kuadithiwa.

Aneth Kushaba AK 47(katikati) akiimba na waimbaji wenzake wa bendi ya Skylight ambao ni Ashura Kitenge(kushoto) na kulia ni John Music kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiimba na kucheza moja ya Sebene la Kikongo pamoja Sony Masamba.
Sony Masamba ambaye ni mmoja wa waimbaji wa Skylight akiendelea kutoa burudani huku akisindikizwa na waimbaji wenzake kulia ni Sam Mapenzi na kushoto ni Joniko Flower.
Waimbaji wa Skylight Band wakiimba kwa moja ya nyimbo za bendi yao kwenye kiota cha Thai Village ijumaa iliyopita.
Sugua sugua mpaka itakate......Waimbaji wa Skylight Band wakicheza moja ya style zao zinazobamba mujini.
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiimba sambamba na msanii mwenzake Sam Mapenzi kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Burudani ikiendelea kutolewa na wasanii wa Skylight Band.
Ashura Kitenge akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band huku akisindikizwa na Aneth Kushaba AK 47(kushoto) pamoja na John Music (kulia)
Sugua Sugua mpaka utakate njoo leo ujifunze kusugua kama hawa mashabiki wa Skylight walivyojua mmoja ya Style ya kusugua
Sam Mapenzi akiendelea kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight band (hawapo pichani) huku akisaidiwa na waimbaji wenzake wa kwanza kushoto ni Ashura Kitenge akiwa smambamba na Sony Masamba(wa pili kutoka kushoto) pamoja na John Music (wa kwanza kulia) kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Ni mwendo wa Kusebeneka mpaka kieleweke kwa mashabiki na wapenzi wa Skylight Band
Ni happy mwanzo mwisho kwa mashabiki wa Skylight.
Mmoja wa mashabiki wa Skylight band akiogeshwa kwa vinywaji wakati wa kusherekea siku yake ya kuzaliwa kwenye kiota hiki cha Thai Village wakati band ya Skylight ikiendelea kutoa burudani.
Kumbukumbu zikichukuliwa hapa tunaweza kusema mpiga picha kapigwa picha
Wakati Sam Mapenzi akiimba wimbo wa "All of Me" mdada huyu ulimgusa sana mpaka akashindwa kujizuia akaamua afanye ya kwake.
Mdada akichukua selfie na msanii wa Skylight Band Sum Mapenzi baada ya kumkuna na weimbo wa "All of Me"

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.