ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 15, 2015

AJALI NYINGINE TENA;BASI LA JORDAN LAPINDUKA NZEGA,LIKITOKEA JIJINI MWANZA KWENDA ARUSHA.

Mtu mmoja amefariki dunia huku wengine 25 wakijeruhiwa katika ajali ya basi la abiria la Jordan lenye usajili wa namba T 650 AQZ lililokuwa likitoka jijini Mwanza kwenda mkoani Arusha na kupinduka leo wilayani Nzega,Tabora.Mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana. 
 Ni taswira ya eneo la ajari huku baadhi ya abiria walio salimika wakifanya utaratibu wa kuwasiliana na ndugu kutoa taarifa ya ajali.
 Baadhi ya Majeruhi wameumia kabisa kama dada huyu kulia ikiwa ni mara baada ya ajali hiyo kutokea. Baadhi ya Abiria wakiwa nje ya basi la Jordan mara baada ya kupinduka wilayani Nzega mkoani Tabora na kupelekea kifo cha mtu mmoja. 

Mmoja wa abiria akifanya mawasiliano baada ya kunusurika kifo basi la Jordan mara baada ya kupinduka wilayani Nzega mkoani Tabora na kupelekea kifo cha mtu mmoja.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.