SAFARI LAGER YATANGAZA BAR 5 ZILIZOINGIA FAINALI NYAMA CHOMA
MWANZA 2015.
Dar es Salaam, Jumanne3 Machi2015: Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza bar tano zilizofanikiwa
kuingia fainali kwenye kinyang’anyiro cha shindano lauchomaji nyama Mkoani Mwanza
lijulikanalo kama “Safari Lager Nyama
Choma Competition 2015”.
Akizungumza na waandishi wa habari,
Meneja matukio wa Tbl Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela alizitaja bar zilizoifanikiwa kuingia fainali
kuwa ni;
1.Victoria Prince Hotel.
2.Shooters Bar.
3.Lunala Bar.
4.SD Excutive Bar.
5.Gemstone Bar.
Alisema Mwayela fainali za
mashindano ya Safari Nyama Choma mwaka huu wa 2015 zinatarajiwa kufanyika
katika Uwanja Furahisha hapa jijini Mwanza kuanzia saa mbili asubuhi na
kuendelea zikisindikizwa na Jambo Star Bend pia ni bendi yetu ya hapahapa Mwanza, DJ mkali kutoka
jijini Dar es Salaam na burudani zingine nyingi pamoja na zawadi kemkem kutoka
Safari Lager..
Shindanohili hufanyika kila mwaka,
na kwa mwaka huulinafanyika kwa mara ya nane
mfululizo na mwaka huu mkoa wetu tumekuwa wa pili kuyafanya mashindano hayo
ambayo yalizinduliwa rasmi Mkoani Mbeya wiki iliyopita
Na baada ya mkoa wa mwanza yataelekea Arusha
,Moshi na baadae jijini Dar es Salaam.
Tangu lilipoanzishwa mwaka 2008,
shindano hili limekuwa na mvuto wa kipekee kwa wanywaji wa bia ya Safari Lager
kwani wamejitokeza kwa wingi kupigia kura baa zao kuhakikisha zinaibuka na
ushindi katika mkoa waliopo.
Kwa mwaka huu mchakato wa kuzipata
bar zilizoingia fainali ilikuwa ni wa kuipigia kura bar unayoipenda wewe mlaji
wa nyama choma kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno kutumia simu za mkononi kwenda
namba0653-215151. Ujumbe ambao ulitozwa
gharama ya kawaida za kutuma ujumbe.
Alisema Erick“Lengo kuu la shindano
la Safari Lager Nyama Choma ni kuongeza
hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze
kufahamu viwango bora vya uchomaji na utayarishaji wa nyama choma. Tunahakikisha
wachoma nyama katika baa za mikoa yote inayoshiriki wanapata elimu na ueledi wa
kutosha katika fani hii ili kumpa mlaji ubora anaostahili kila anapokula nyama
choma.
Tumezingatia maombi ya washiriki
mwaka jana hivyo basi mwaka huu semina inayoelekeza namna nzuri ya uchomaji
nyama itafanyika kwa bar zote zinazoshiriki na wala sio baa chache
zilizochaguliwa kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma”. Erick aliendelea kufafanua
kwamba, washiriki watapimwa ujuzi wao katika kutayarisha nyama choma za aina
tatu; nyama ya ng’ombe, nyama ya mbuzi na nyama ya kuku.
“Safari Lagertutaendeleakujitahidikuhakikishawatejawetuwanapatahuduma
bora yanyamachoma. Tunawaombasanawashirikikutumiavizurielimunauzoefuwanaopatailikuongezauborawautayarishajiwanyamachomakwawatejawetu.
MashindanohayayaSafari Lager NyamaChomayatakosamaanasahihiendapowachomanyamawatakuwawanashirikikwalengo
la kujipatiamanufaabinafsinakusahauyaleyotewaliyojifunzahadimwakamwingine”.Shindalo
la mwakahuulinaongozwanakibwagizo…. Safari
Lager naNyamaChomandioMpangomzima!.AlisemaAbuu.
Mwisho Erick alitaja zawadi za mwaka
huu kuwa ni;
1.Bingwa wa
Mkoa...................1,000 000/= pamoja na Kikombe
2.Mshi wa pili
...........................800,000/=
3.Mshindi wa
tatu........................600,000/=
4.Mshindi wa
nne........................400,000/=
5.Mshindi wa
tano.......................200,000/=
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.