ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 13, 2015

PPF MKOA WA MWANZA YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 NA MABATI 100

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akisalimiana na meneja wa PPF Kanda ya Ziwa Mesharck Bandawe pindi alipowasili jana Kahma mkoani Shinyanga kutoa pole kwa waathirika wa mvua zilizoambatana na upepo eneo la Mwakata wilayani humo.
Rais Jakaya Kikwete amesema serikali inatafuta fedha za kujenga nyumba 468 mpya za kisasa na kukarabati nyumba zilizoezuliwa na upepo katika eneo la Mwakata huko Kahama mkoani Shinyanga pamoja na kuendelea kuhudumia waathrika wote kwa chakula, malazi na dawa hadi watakapopata makazi bora ya kudumu. 
Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa Meshack Bandawe akitoa taarifa kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi, Mabati 112 na mifuko ya simenti 100 msaada wenye jumla ya thamani ya shilingi milioni tatu za kitanzania.
Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa Meshack Bandawe (kulia) akikabidhi msaada wa simenti na mabati kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya kwaajili ya wahanga wa mvua kubwa iliyonyesha wiki iliyopita katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama na kusababisha watu 649 kukosa mahali pa kuishi. 
Jumla ya mabati 112 yamekabidhiwa kama sehemu ya msaada.
Nayo mifuko 100 ya simenti ni sehemu ya msaada toka PPF.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya (kushoto) akitoa shukurani kwa PPF kupitia Meneja wake Kanda ya Ziwa Meshack Bandawe (kulia) mara baada ya kukabidhiwa msaada wa simenti na mabati kwaajili ya wahanga wa mvua kubwa iliyonyesha wiki iliyopita katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama na kusababisha watu 649 kukosa mahali pa kuishi. 
PPF. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa na wilaya kutembelea maeneo ya kata za wahanga wa mvua kubwa iliyonyesha wiki iliyopita katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama na kusababisha watu 649 kukosa mahali pa kuishi. 
Ukuta umeanguka paa liko mashakani.
Hali tete.
Salaaam .....poleni. 
RAIS Jakaya Kikwete amesema Serikali itajenga nyumba 403 ambazo zimebomolewa na mvua kubwa iliyonyesha wiki iliyopita katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama na kusababisha watu 649 kukosa mahali pa kuishi.


Kauli hiyo aliitoa jana kwenye kijiji cha Mwakata baada ya kutembelea eneo lililoathiriwa na mvua hiyo na kujionea maisha duni wanayoishi watu hao.


Akizungumza na wananchi waliohudhuria mkutano wake Rais Kikwete alisema Serikali iko pamoja na wananchi hao na itahakikisha makazi yao yanarejea katika hali yake ya kawaida kwa kuwajengea nyumba hizo.


Pia, Rais Kikwete aliagiza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wajenge nyumba hizo bila kupitia mkandarasi yeyote kama vile ulivyo ujenzi wa Serikali kwa kuwa ujenzi wa jeshi unaisha kwa muda mfupi na hakuna uchakachuaji.


Aliwataka viongozi mkoani Shinyanga kuhakikisha ujenzi huo hautangazwi na kuagiza JKT kwenda kwenye eneo hilo kufanya tathmini ya ujenzi huo ili uanze mara moja.


Rais Kikwete aliwatoa wasiwasi wananchi wa Mwakata waliokumbwa na tatizo hilo kwamba Serikali itahakikisha wote wamepata chakula hadi mwisho watakapolima na kupata mavuno na tukio hilo wasilihusishe na imani za kishirikina.


Alisema mvua hizo ni za kawaida ambazo hutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na si ushirikina hivyo aliwataka wananchi hao waendelee kuwa na hisia hizo lakini wasilichukulie kwa uzito swala la ushirikina wakatafuta mchawi wa mvua hiyo


Awali, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga alimwambia Rais Kikwete kwamba mvua hiyo licha ya kuua watu 47 pia imeharibu mazao hekari 2,332 pamoja na visima 53 vya maji ya kunywa.


Rufunga alisema mpaka kufikia sasa wahisani mbalimbali wamechangia kwenye tukio hilo Sh64 milioni pamoja na tani 63 za unga wa sembe pamoja na mahitaji mbalimbali ya kibinadamu yakiwamo mabati zaidi ya 1,000

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.