ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 5, 2015

NYAMA CHOMA MWANZA NI JUMAMOSI HII

SAFARI LAGER YATANGAZA  BAR 5 ZILIZOINGIA FAINALI  NYAMA CHOMA  MWANZA 2015.
Dar es Salaam, Jumanne3 Machi2015: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza bar tano zilizofanikiwa kuingia fainali kwenye kinyang’anyiro cha shindano lauchomaji nyama Mkoani Mwanza lijulikanalo kama “Safari Lager Nyama Choma Competition 2015”.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja matukio wa Tbl Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela  alizitaja bar zilizoifanikiwa kuingia fainali kuwa ni;
1.Victoria Prince Hotel.
2.Shooters Bar.
3.Lunala Bar.
4.SD Excutive Bar.
5.Gemstone Bar.

Alisema Mwayela fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma mwaka huu wa 2015 zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja Furahisha hapa jijini Mwanza kuanzia saa mbili asubuhi na kuendelea zikisindikizwa na Jambo Star Bend pia ni bendi  yetu ya hapahapa Mwanza, DJ mkali kutoka jijini Dar es Salaam na burudani zingine nyingi pamoja na zawadi kemkem kutoka Safari Lager..

Shindanohili hufanyika kila mwaka, na  kwa mwaka huulinafanyika kwa mara ya nane mfululizo na mwaka huu mkoa wetu tumekuwa wa pili kuyafanya mashindano hayo ambayo yalizinduliwa rasmi Mkoani Mbeya wiki iliyopita
 Na baada ya mkoa wa mwanza yataelekea Arusha ,Moshi na baadae jijini Dar es Salaam.
Tangu lilipoanzishwa mwaka 2008, shindano hili limekuwa na mvuto wa kipekee kwa wanywaji wa bia ya Safari Lager kwani wamejitokeza kwa wingi kupigia kura baa zao kuhakikisha zinaibuka na ushindi katika mkoa waliopo.

Kwa mwaka huu mchakato wa kuzipata bar zilizoingia fainali ilikuwa ni wa kuipigia kura bar unayoipenda wewe mlaji wa nyama choma kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno kutumia simu za mkononi kwenda namba0653-215151. Ujumbe ambao ulitozwa gharama ya kawaida za kutuma ujumbe.

Alisema Erick“Lengo kuu la shindano la Safari Lager Nyama Choma ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango bora vya uchomaji na utayarishaji wa nyama choma. Tunahakikisha wachoma nyama katika baa za mikoa yote inayoshiriki wanapata elimu na ueledi wa kutosha katika fani hii ili kumpa mlaji ubora anaostahili kila anapokula nyama choma.

Tumezingatia maombi ya washiriki mwaka jana hivyo basi mwaka huu semina inayoelekeza namna nzuri ya uchomaji nyama itafanyika kwa bar zote zinazoshiriki na wala sio baa chache zilizochaguliwa kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma”. Erick aliendelea kufafanua kwamba, washiriki watapimwa ujuzi wao katika kutayarisha nyama choma za aina tatu; nyama ya ng’ombe, nyama ya mbuzi na nyama ya kuku.

 “Safari Lagertutaendeleakujitahidikuhakikishawatejawetuwanapatahuduma bora yanyamachoma. Tunawaombasanawashirikikutumiavizurielimunauzoefuwanaopatailikuongezauborawautayarishajiwanyamachomakwawatejawetu. MashindanohayayaSafari Lager NyamaChomayatakosamaanasahihiendapowachomanyamawatakuwawanashirikikwalengo la kujipatiamanufaabinafsinakusahauyaleyotewaliyojifunzahadimwakamwingine”.Shindalo la mwakahuulinaongozwanakibwagizo…. Safari Lager naNyamaChomandioMpangomzima!.AlisemaAbuu.

Mwisho Erick alitaja zawadi za mwaka huu kuwa ni;
1.Bingwa wa Mkoa...................1,000 000/= pamoja na Kikombe
2.Mshi wa pili ...........................800,000/=
3.Mshindi wa tatu........................600,000/=
4.Mshindi wa nne........................400,000/=

5.Mshindi wa tano.......................200,000/=

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.