ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 19, 2015

MPAMBANO WA MASUMBWI KUFANYIKA MANYARA PARK 28/3/2015

Na Mwandishi Wetu 
Mabondia Julius Kisarawe kutoka 'Ndame Club' na Saidi Uwezo kutoka 'Mzazi GYM' watapanda uringoni march 28 kugombania ubingwa wa taifa wa kg 54 katika ukumbi wa manyara park uliopo CCM Tandale Manzese mpambano uho wa raundi kumi wenye upinzani wa hali ya juu utasindikizwa na mabondia mbalimbali kutoka katika kambi tofauti

ambapo bondia Ibrahimu Tamba atapambana na George Dimoso na Vicent Mbilinyo kutoka kwa 'Super D Boxing Coach' atapambana na Yusufu Mkari na kasimu Gamboo atakabiliana na Mustafa Dotto na Mohamed Kibanga atapambana na Bakari Dunda wakati Karim Mura  atamkabili Eddy Baguo


Bondia Cosmas Cheka kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa U.B.O Africa utakaofanyika jumamosi ya feb 28 uwanja wa ndani wa taifa picha na SUPER D BOXING NEWS 
Na Mwandishi Wetu 
MABONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Cosmas Cheka wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa raundi kumi kugombania ubingwa wa U.B.O Africa utakaofanyika jumamosi hii katika uwanja wa ndani wa taifa.


Mpambano huo mkali utatanguliwa na ngumi kali kutoka kwa bondia Fransic Miyeyusho atakaezipiga na Fadhili Majiha mpambano wa raundi nane mpambano mwingine wa ubingwa ni kati ya Alibaba Ramadhani na Jacobo Maganga.

Katika kusindikiza mapambano hayo makali bondia machachari na chipkizi Vicent Mbilinyi ataoneshana umwamba na Epson John wa Morogoro na Shomari Milundi atapambana na Mwinyi Mzengela huku Husein Mbonde atakabiliana na Shedrack Ignas.

Katika kuhakikisha mpambano huo unakuwa wa kihistoria na kuacha gumzo nchini bondia Said Mundi wa Tanga atapambana na Ramadhani Shauli na mapambano mengine mbalimbali.

Mpambano huo unaosimamiwa na P.S.T chini ya rais wake Emanuel Mlundwa yamekuwa gumzo mjini na kusababisha taflani za mabondia kutaka kupigana kavukavu uku makocha wao pia wakikunjiana ngumi 
siku hiyo kutakuwa na ulinzi na usalama wa kutosha kwa watu na mali zao  


siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.