Bi Emiliana ni mfanya biashara ndogo ndogo na mkazi wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara akishuhudia ni meneja mauzo wa Airtel kanda ya kaskazini bwana Brighton Majwala |
Wakazi wa wawili wa wilaya ya Hanang Mkoani Manyara kwa pamoja wamezawadiwa magari yao aina ya Toyota IST mara baada ya kuibuka washindi katika droo za promosheni ya Airtel yatosha Zaidi inayoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
Mpaka sasa jumla ya washindi 37 wameshapatikana kutoka katika mikoa mbalimbali ikiwa bado promosheni inaendelea na magari mengi bado yanasubiri washindi ili wakabithiwe akiongea wakati wa halfa ya kukabithi magari kwa wateja wa Airtel Mkoani Manyara, Meneja wa Airtel Kanda ya Kaskazini Bwana Brighton Majwala alisema "Tunajisikia furaha kuendelea kupata washindi wa rika tofauti kutoka katika maeneo mbalimbali nchini, nasikia furaha kupata washindi kutoka katika kanda yangu na hivyo naendelea kuwaasa watumiaji wa mtandao wa Airtel na wale ambao hawajajiunga kufanya hivyo na kupata nafasi ya kujishindia.
Promosheni bado inaendelea na magari bado yapo kinachotakiwa kufanya ni kununua na kujiunga na kifurushi chako cha Airtel yatosha zaidi na kupata nafasi ya kujishindia.
Nawapongeza sana washindi wetu wa leo na washindi wote ambao wameshapatikana mpaka sasa, na nachoweza kusema ni kwamba Airtel tunajivunia kuwa sehemu ya kubadili maisha ya watanzania wengi hasa walio na kipato cha chini na kuwawezesha kufikia ndoto zao huku tukiendelea kurahisisha shughuli zao za kiuchumi na kijamii kupita huduma zetu na promosheni kama hizi. ni matumaini yetu kwa kupitia promosheni hii ya Airtel yatosha zaidi watanzania wengi wataguswa na kuboreshewa maisha yao.
Kwa upande wake Bwana Mohamed Ahmad Khamis ambaye ni mshindi wa gari aina ya Toyota IST alisema" nimesikia furaha kubwa sana leo kupata ushindi huu mkubwa, kwangu hii imekuwa kama ndoto, mimi ni mtumiaji mzuri sana wa huduma za Airtel na ninazo line tatu za Airtel na hii moja leo imenipa ushindi. kwakweli nimeamini kabisa Airtel yatosha zaidi na inabadilisha maisha ya watanzania,
"Nimekuwa na ndoto za kumiliki gari lakini leo Airtel imeniwezesha kufikia malengo yangu na kunipa ushindi huu mkubwa na kuniwezesha kumiliki gari langu, nawashauri watanzania hasa wale wasioamini kuhusu promosheni hizi sasa waamini na kujua kwamba ni kweli promosheni hii na ni ya uhakika kwani mimi nimeshinda bila kuwa na taarifa yeyote. nawashukuru sana Airtel yatosha zaidi naye mama Emiliana Tarmo Hhaway ambaye alizidiwa na furaha hadi kushindwa kuongea kwa lugha ya kiswahili alisema.
"Namshukuru Mungu sana kwa kuniwezesha kushinda gari hili lakini pia nawashukuru sana Airtel kwa kuniwezesah kushinda. mimi nimenunua kifurushi cha Airtel yatosha cha shilingi mia tano na leo namiliki gari la mamilioni ya pesa ni jambo la kustaajabu sana.
Gari hili sasa litaniwezesha katika shughuli zangu za kilimo, kutoa mazao shambani kwenda sokoni, litanisaidia katika shughuli zangu za kijamii, kusaidia majirani hasa tukiwa na wagonjwa na nyingine nyingi. nasema asante sana kwa Airtel na kwa ushindi huu Droo ya wiki ya 7 ya promosheni ya Airtel Yatosha inategemea kufanyika siku ya Alhamisi jioni ambapo washindi wengine 7 wa wiki hii watapatikana na kutangazwa
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.