ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, February 15, 2015

TOTO YAUNGANA NA MWADUI KUPANDA LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA

Toto Africans yapanda ligi kuu soka Tanzania bara mwaka 2015 baada ya kuifunga Rhino Rangers ya Tabora bao 2-0. Mchezo uliohezwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
HATIMAYE Wanakishamapanda timu ya Toto Africans ya jijini Mwanza imeungana na timu ya Mwadui Fc ya mkoani Shinyanga, Africans Sports ya mjini Tanga na Majimaji ya Songea kuingia Ligi kuu soka Tanzania bara. ZAIDI BOFYA PLAYA KUSIKILIZA KILICHOJIRI. 
Kikosi cha Rhino Rangers.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula akisalimiana na wachezaji wa timu ya Rhino Rangers, kabla ya mchezo na Toto uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Msanii maarufu wa Filamu nchini Steve Nyerere akisalimiana na mchezaji wa Toto Africans Emma Swita kabla ya mchezo dhidi ya Rhino Rangers, uliochezwa kuhitimisha Ligi soka daraja la kwanza Tanzania Bara ambapo Toto Africans iliibuka na ushindi wa 2-0 na kurajea Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.
Meza kuu na salamu zao kabla ya mchezo.
Team captain wa timu zote mbili na waamuzi.
Mchezo ukiendelea.
Mashabiki wa Toto Africans wakishangilia goli la Kwanza lililofungwa dakika ya 15 na Jafari Mohamed.
Ni goli la pili na hapa Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula (mwenye skafu) akijumuika na Mwenyekiti wa Chama Cha Soka mkoa wa Mwanza Jackson Songora (wa kwanza kushoto) kushangilia, kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Hassan Hida akifuatiwa na Meya wa Manispaa ya Ilemela Henry Matata. 
Mwendo wa kushangilia.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula akifungua shampein kushangilia Toto Africans kurejea Ligi kuu.
Benchi la Toto.
Mashabiki na shangwe zao.
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya H. Baba alikuwa ni mmoja kati ya wachagizaji ushindi kwa timu yake ya nyumbani Toto Africans.
Hureeee....!!
H Baba na Bendera ya Toto.
Picha ya pamoja ....

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.