ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 9, 2015

RUSHWA ADUI WA KILA SEKTA.

Mhandisi wa Ofisi ya Katibu Tawala (RAS) Mkoa wa Iringa,David Michae, akila kiapo cha Uhandisi mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana, Suniva Mwanjombe, wakati wa mkutano mkuu wa wahandisi jijini Mwanza.
Mhandisi wa Ofisi ya Katibu Tawala (RAS) Mkoa wa Iringa,David Michae, akisaini kiapo cha Uhandisi mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana, Suniva Mwanjombe, wakati wa mkutano mkuu wa wahandisi jijini Mwanza.
Mhandisi wa Ofisi ya Katibu Tawala (RAS) Mkoa wa Iringa,David Michae, akikabidhiwa Hati ya kiapo cha Uhandisi na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana, Suniva Mwanjombe, wakati wa mkutano mkuu wa wahandisi jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Association of Local Government Engineers in Tanzania (ALGETA), Gerald Matindi, akichangia mada kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa Wahandisi wa Serikali za Mitaa unaofanyika jijini Mwanza.

NA PETER FABIAN, MWANZA.
WAHANDISI wameaswa na kukumbushwa kutojihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo ya Halmashauri zao na kujihusisha na vitendo  vinavyoweza kuchangia kupata ugonjwa hatari wa Ukimwi.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwakirishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Ndalo Kulwijira, hivi karibuni wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wahandisi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jijini Mwanza, alisema rushwa inatakiwa kupigwa vita kwa nguvu zote na bila kuwaonea haya .

“Rushwa imekuwa ikitolewa kwa watumishi wa umma na baadhi ya watu wanaoshinda zabuni za Serikali na Halmashauri za Majiji, Manispaa, Wilaya na Miji wakati wa utekelezwaji miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo hutoa huduma kwa wananchi jambo hili limekuwa likirudisha nyuma maendeleo na upatikanaji huduma bora,”alisema.

Kulwijira alisema kwamba rushwa ni adui kwa kila mtu hivyo ni vyema watumishi wa umma wakajikita kutekeleza majukumu ya taaluma zenu kwa weledi na kuzingatia taratibu, sheria na viapo vyenu ili kuondoa manuguniko miongoni mwa jamii kwa serikali yao iliyopo madarakani.

Aidha Kulwijira aliongeza kuwa tayari serikali ilitoa walaka maalumu kwa watumishi wa umma na kuagiza kupitia wizara ya TAMISEMI kwa wakurugenzi wote wa Halmashauri nchini washughulikie kikamilifu na kupiga vita rushwa kwa nguvu zote katika maeneo yao ya kazi wakati wa utekelezaji wa miradi ya miundombinu.

“Tumeisha chukua hatua sitahiki za kuunda Kamati katika kila Halmashauri zenu ambapo baadhi ya wahandisi ni wajumbe, tunachowaomba ni kuzisaidia ili ziweze kupambana rushwa ili kuhakikisha Halmashauri zenu zinatekeleza miradi ya maendeleo, kuweesha kutoa huduma bora kwa jamii na majukumu yake ipasavyo,”alisisitiza.

Kulwijira aliwakumbusha na kuwaeleza watumishi hao wa umma kuwa Ukimwi bado ni janga ambalo linamaliza nguvu kazi ya Taifa hili, hatuna budi kushirikiana kulitokomeza , wahandisi wanapokubwa na kupata ugonjwa huu na kusababisha kifo cha mhandisi mmoja basi taifa linakuwa sawa limepoteza wahandisi 10.

Akitoa neon la shukurani wakati wa mkutano huo, Mhandisi Juliana James alisema kuwa ushauri uliotolewa pamoja na maagizo ya serikali kwa wahandisi yatachukuliwa na kufanyiwa kazi ili kuepusha watumishi wa umma kushiriki vitendo vya rushwa na changamoto zake ikiwemo kujikinga na Ukimwi.

Mhandisi James, alisema Wahandisi walioshiriki mkutano mkuu wa mwaka wa tisa wa Assiocition of Local Government Engineers in Tanzania (ALGETA) kutoka Halmashauri za Serikali za Mitaa nchini uliolenga kujadili kwa kina utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji huduma bora za Kihandisi (taaluma ya Uhandisi) kwa maendeleo ya jamii. 

Aidha Mkutano huo na mchango wa ALGETA katika ustawi na maendeleo ya Serikali za Mitaa unatoa fursa muhimu kwa watendaji kwenye utekelezaji wa majukumu ya msingi ya serikali ya awamu ya Nne iliyolenga kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2005, MKUKUTA, Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 na lengo la Milenia ya Umoja wa Mataifa kwa mafanikio makubwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.