Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde. |
Wanahabari toka Sahara Media. |
Airtel yazindua promosheni ya Airtel yatosha Zaidi kwa Wakazi wa Mwanza
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi kwa wakazi wa Mwanza wakati ziara yake yenye lengo la kuwaelimisha wateja wake juu ya promosheni hiyo kambambe inayowawezesha wateja wake kujishindia gari Aina ya Toyota IST kila siku
Promosheni ya Airtel yatosha Zaidi iliyozinduliwa Jumatatu wiki iliyopita mpaka sasa imewawezesha wateja wa 3 kutoka katika mikoa mbalimbali kujishindia magari aina ya Toyota IST kufatia droo iliyochezeshwa ijumaa iliyopita chini ya usimamizi wa bodi ya mchezo ya kubahatisha Tanzania
Akiongea kwa niaba ya Airtel Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” Tunayofuraha kuitambulisha kwenye wakazi wa mkoa wa Mwanza promosheni yetu ya Airtel Yatosha Zaidi ninayomuwezesha wateja wetu kuendelea kufurahia vifurushi vya huduma ya Airtel yatosha huko wakijishindia Toyota IST Moja kila siku. Mpaka sasa tunao washindi wa tatu ambao wamepatikana kupitia droo iliyochezeshwa siku ya Ijumaa iliyopita, wewe pia unayo nafasi ya kuibuka mshindi kwa kujiunga tu na vifurushi vya Airtel yatosha vya siku, wiki au Mwezi namba yako itaingia moja kwa moja kwenye droo, hakuna makato yoyote wala gharama ya ziada ni kwa matumizi yako yakaawaida ya kila siku tunakuwezesha kushinda zawadi nono.
Akitangaza majina ya washindi Bi Jane Matinde alisema washindi wetu katika droo yetu ya kwanza ni pamoja na Ramadhani Dilunga, Mkulima Mkazi wa mkoa wa Pwani, Namtapika Kilumba, mwalimu Mstaafu na mkazi wa mkoa wa Mtwara pamoja na Mwajabu Churian , mfanyabiashara na mkazi wa Mbagala Jijini Dar es Saalam. Bado kuna magari 57 yamebaki kwa wewe mteja wa Airtel kujishindia
Natoa wito kwa wakazi wa Mwanza na watanzania kwa ujumla kujiunga katika vifurushi hivi kwa kupiga *149*99* au kwa kununua Vocha ya Airtel Yatosha au kwa kupitia huduma ya Airtel Money na kupata vifurushi vya sms, muda wa maongezi na internet zaidi kulinganisha na zifurushi vingine sokoni lakini zaidi Airtel yatosha inakupati nafasi ya kushinda Toyota IST kila siku aliongeza Matinde
Kwa upande wake mkazi wa Mwanza Bwana Selestine Bundala alisema” tumefurahia sana promosheni hii kwani inatupa nafasi ya kujishindia bila kutuma ujumbe mfupi wala kujibu maswali lakiini zaidi inampaita mshindi gari la kisasa na kumwezesha kufanya shughuli zake kirahisi, nawapongeza Airtel sana na mimi pia naendelea kuvitumia vifurushi hivi kwani vinarahisisha huduma za mawasiliano na kuzifanya kuwa za gharama nafuu.
Droo ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha zaidi itafanyika ijumaa hii ambapo washindi saba wa wa wiki hii watatangazwa. Na washindi watatu wa wiki iliyopita watabithiwa magari yao siku ya Jumatano.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.