ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 11, 2015

MAZISHI YA MZEE JESTUS BULUGU MAPESA YAFANYIKA MAGU JIJINI MWANZA

Wachungaji na wakuu wa kanisa la AICT wakifanya ibada kuuombea mwili wa Marehemu Jestus Bulugu Mapesa, iliyofanyika jana katika kijiji cha Kinango wilayani Magu mkoani Mwanza.
Sehemu ya ndugu, watu wa karibu wa familiaya marehemu Mzee Mapesa wakiwa katika maombolezo.


Familia ya Marehemu Mzee Jestus Mapesa Kutoka kshoto ni Peter Mapesa (mtoto wa tatu wa marehemu), akifuatiwa na dada Lucy (wa pili kuzaliwa), kaka God Mapesa (wa kwanza kuzaliwa) na mjane Mrs. Mapesa, wakishiriki ibada.


Sehemu ya waombolezaji waliofika katika kijiji cha Kinango wilayani Magu kuhudhuria mazishi ya Mzee Mapesa.
Mzee Simbira (wa tatu kutoka kushoto) ni mmoja kati ya wazee wakongwe wa jiji la Mwanza naye alisafiri hadi katika kijiji hiki kwaajili ya kushiriki ibada ya mazishi ya Marehemu Jestus Bulugu Mapesa.
Peter Mapesa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa baba yake marehemu Jestus Mapesa aliyefariki mnamo tarehe 6/feb/2015 katika hospitali ya Rufaa Bugando ambako alikuwa akiugulia maradhi ya kupooza mwili, yaliyomsumbua kwa takribani muda wa miaka mitano.
Leah G. Sengo akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu baba yake mkubwa Jestus Mapesa aliyefariki mnamo tarehe 6/feb/2015 katika hospitali ya Rufaa Bugando ambako alikuwa akiugulia maradhi ya kupooza mwili, yaliyomsumbua kwa takribani muda wa miaka mitano.
Mrs. G. Sengo akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mzee Mapesa aliyefariki mnamo tarehe 6/feb/2015 katika hospitali ya Rufaa Bugando ambako alikuwa akiugulia maradhi ya kupooza mwili, yaliyomsumbua kwa takribani muda wa miaka mitano.




Msafara kuelekea hatua ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Mzee Mapesa.


Picha ya pamoja ya familia.
Gari lililoubebe mwili wa marehemu likiwa tayari kuelekea makaburini.
Mwili wa marehemu Jestus Mapesa ukishushwa kwenye nyumba yake ya milele.
Ibada ya mwisho.
"Uliumbwa kwa udongo na mavumbini  utarudi"
Mke wa marehemu akiweka shada la maua.
Kaka na wadogo zake marehemu.
Kanisa likiwakilisha. 
Makaburi ya ukoo katika shamba la familia ya Mapesa kijiji cha Kinango wilayani Magu, hapa ndipo mahala alipozikwa Jestus Bulugu Mapesa. 
Mara baada ya mazishi kukamilika ndugu jamaa na marafiki walirejea nyumbani na kufarijiana.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.