ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, January 11, 2015

VURUGU ZA TIMU YA POLISI DODOMA ZAVUNJA MCHEZO BAINA YAO NA TOTO AFRICANS


NA. ALBERT G.SENGO: MWANZA

Bado vitendo vya kutumia ubabe na mamlaka ya rasilimali jeshi ili kupata matokeo kwa baadhi ya timu zinazomilikiwa na Jeshi la Polisi toka mikoa tofauti tofauti hapa nchini hususani zinazoshiriki Ligi soka daraja la kwanza Tanzania Bara vimeendelea kutawala, kushamiri na kuwa sugu kiasi cha kuondosha ladha na makusudio ya mchezo wenyewe.

Hilo limeonekana kwenye mchezo uliofanyika leo (jumapili) baina ya Toto Africans na Polisi Dodoma uliovunjika katika dakika ya 70, Toto wakiongoza kwa bao 1-0, ikiwa ni mara baada ya baadhi ya wachezaji wa Polisi Dom na viongozi benchi la ufundi kumdunda refa na kamisaa wa mchezo huo. (SIKILIZA TAARIFA YA SPORTS XTRA)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.