NA ALBERT G. SENGO MWANZA.
KESHO katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kutakuwa na pambano la soka mchezo wa kirafiki wakimataifa ulio katika kalenda ya FIFA kati ya Taifa Stars (Maboresho) dhidi ya timu ya Taifa ya Rwanda 'Amavubi'.
Tayari timu zote zimeshawasili jijini Mwanza, Taifa Stars wakitangulia tangu majuzi nao Amavubi wakiwasili hii leo jioni majira ya saa 16:00 na ndege ya Shirika la Fast Jet, kikosi kikiwa na watu 27, wakiwemo wachezaji 20 na viongozi 7.
Vicent Mashami ni kocha Msaidizi wa Kikosi cha timu ya Taifa cha Rwanda 'Amavubi' akizungumza na Sports Xtra amewaahidi wapenzi wa soka watakao tinga uwanja wa CCM Kirumba kushuhudia kandanda safi la kuvutia, huku akisema kuwa anaamini kikosi cha Taifa Stars kitaipa changamoto timu yake kutokana na historia ya kuwa na wachezaji wazuri. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.