Kwa mara ya kwanza ikicheza nyumbani Stand United hii leo imeonja utamu wa ligi kuu soka Tanzania bara mara baada ya kupata ushindi wake wa kwanza ndani ya ligi hiyo kwa kuifunga Mbeya City 1-0 mchezo ukichezwa dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Mashabiki wa Mbeya City walikuwa na mbwembwe kiasi cha kuliweka kiganjani dimba hilo nao mashabiki wa Stand wakiwa kama wamenyeshewa mvua kwa muda wa takribani dakika 45 za kipindi cha kwanza na dakika kama 15 za kipindi cha pili lakini mambo yalibadilika baada ya hapo furaha yao ikageuka kuwa kilio.
Mbwembwe mwanzo mwisho...lakini mwisho wa mchezo Mbeya City wanatoka vichwa chini...
Dakika ya 76 Shangwe za mashabiki wa Stand United zatawala safari hii zikiwa na maana zaidi baada ya mshambuliaji wa timu hiyo Chibibiere Abisalum, ambaye ni raia wa Nigeria kupasia mpira kambani akipokea pande safi toka kwa Musa Said Kimbu aliye wapunguza mabeki wa Mbeya City.
ENDORO WATER FALLS, MAAJABU MENGINE NGORONGORO
-
Mbaraka Mwinshehe aliwahi kuimba akiisifia Morogoro na jinsi maji
yanavyotiririka kutoka milimani.
Mwinshehe angekuwa hai pengine angefika maporomoko ...
Rais Museveni atangazwa mshindi wa uchaguzi Uganda
-
Tume ya uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Kaguta Museveni kama
mshindi wa uchaguzi uliofanyika Alhamisi wiki hii, akiwa na jumla ya kura
7,946...
0 comments:
Post a Comment