ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 10, 2014

HIZI HAPA MBIO ZA MITUMBWI MWANZA

Baadhi ya Wakimbia mbio za Makasia Wanaume wakichuana wakati wa fainali za mbio za Mitumbwi zinazodhaminiswa na Bia ya Balimi Extra Lager zijulikanazo kama “ Balimi Boat Race 2014” Mkoa wa Mwanza zilizofanyika mwishoni mwa wiki ambapo kikundi cha Costantine Lusalage kutoka Sengerema kilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mkoa upande wa Wanaume.
Chapa makasia....
Chapa vuja jasho upate ushindi....
Pilika pilika...
Mshike mshike....
Baadhi ya Wakimbia mbio za Makasia wanaume ndani ya ushindani kusaka ngawira.
Baadhi ya Wakimbia mbio za Makasia Wanawake wakichuana wakati wa fainali za mbio za Mitumbwi zinazodhaminiswa na Bia ya Balimi Extra Lager zijulikanazo kama “ Balimi Boat Race 2014” Mkoa wa Mwanza zilizofanyika mwishoni mwa wiki ambapo kikundi cha Joyce Alon kutoka Misungwi kilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mkoa upande wa Wanawake.
Meneja wa bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa(kulia) akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa mbio la Mitumbwi zilizodhaminiwa na bia  hiyo zilizofanyika Mwanza mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Meneja Masoka wa TBL Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki.
Washindi wa kwanza Wanawake  wa mbio za Mitumbwi, kikundi Joyce Alon kutoka Misungwi Mkoa wa Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa kitita cha pesa taslimu Shilingi 700,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha Mkoa wa Mwanza katika fainali za Kanda zinazotarajiwa kufanyika Mkoani humo Desemba 6,2014.
Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ilemela,  akimkabidhi Nahodha wa kikundi cha Constatine Lusalage kutoka Sengerema Mkoani Mwanza pesa taslimu Shilingi 900,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda mara baada ya kuibuka mabingwa wa mkoa wa mbio hizo za makasia zilizofanyika mwishoni mwa wiki Mkoani humo.
Washindi wa kwanza Wanaume  wa mbio za Mitumbwi, kikundi Costantine Lusalage kutoka Sengerema Mkoa wa Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa kitita cha pesa taslimu Shilingi 900,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha Mkoa wa Mwanza katika fainali za Kanda zinazotarajiwa kufanyika Mkoani humo Desemba 6,2014.
KIKUNDI CHA COSTANTINE LUSALAGE MABINGWA MBIO ZA BALIMI MITUMBWI MWANZA.
Na Mwandishi wetu, Kagera.
KIKUNDI cha Wanaume wapiga kasia cha Costantine Lusalage kutoka Sengerema Mkoani Mwanza kimeibuka na ubingwa wa Mkoa wa fainali za kimkoa mbio za mitumbwi chini ya udhamini wa bia ya Balimi Extra Lager zijulikazo kama “Balimi Boat Race 2014” na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 900,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Mwanza kwenye fainali za  Kanda zinazotarajiwa kufanyika Desemba 6 mwaka huu jijini Mwanza.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha Elisha Jacob kutoka Misungwi ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 700,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda jijini Mwanza pia, wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha Emmanuel Masanyiwa kutoka Luchelele ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 500,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Daniel Genha kutoka Misungwi ambacho kilizawadiwa Shilingi 400,000/=

Nafasi ya tano hadi ya tisa walipewa kifutajasho cha pesa taslimu Shilingi 250,000/= kila kikundi ambavyo ni kikundi cha Mussa Msalaba kutoka Sengerema, Joseph Jacob kutoka Misungwi, Katula Msese kutoka Kigoto, Faustine Daud kutoka Ibanda, Lubongeja Manyasiwa kutoka Sengerema na Simon Salala kutoka Misungwi.

Upande wa Wanawake kikundi cha Joyce Alon kutoka Misungwi kilifanikiwa kutwaa ubingwa na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 700,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda jijini Mwanza. 

Nafasi ya pili Wanawake ilichukuliwa na kikundi cha Tabu Daudi kutoka Misungwi ambao walizawadiwa Shilingi 600,000/=,washindiwa tatu ni kikundi cha Ntabo Hussein kutoka Luchelele ambao walizawadiwa Shilingi 400,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Leah William kutoka Misungwi ambao walizawadiwa Shilingi 300,000/= na nafasi ya tano hadi ya kumi walizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi 200,000/= kila kikundi ambavyo ni kikundi cha Winifrida William kutoka Misungwi, Revina Magafu kutoka Kigoto, Anna Elias kutoka Kigoto, Moshi Maji kutoka Kigoto, Kizuka Kapani kutoka Bwiru na Robby Mwita kutoka Mwaloni.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi Meneja wa bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa  kwanza alishukuru vikundi vyote vilivyojitokeza kushirika mashindano hayo lakini pia aliwapongeza wale wote waliofanikiwa kupata zawadi na kuwaomba waliofanikiwa kupata nafasi ya kuwakilisha Mkoa wa Mwanza kwenye fainali za Kanda wafanye mazoezi ya kutosha na mwisho wasiku ushindi ubaki Mwanza kwa mwaka 2014.

Edith alisema washiriki wote mliofanikiwa kupata zawadi mkatumie vizuri hizo pesa kwa maendeleo yenu na pamoja na maadalizi ya mashindano mengine mwaka ujao.

Fainaliza Kanda zambio za mitumbwi zijulikanazo kama “Balimi Boat Race 2014” zinatarajiwa kufanyika Desemba 6, mwaka huu jijini Mwanza katika ufukwe wa Mwaloni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.