|
Dk. Kigwanga akitiwahutubia wanamichezo. |
|
Dk. Kigwangala Akijumuika katika kufanya Mazoezi. |
|
Dk. Kigwangala akipokea maandamano ya wanamichezo wa Jogging . |
|
Mwenyeikiti Mstaafu wa BMT Dionis Malinzi akitoa neno la Shukran. |
|
Vyeti kwa wanamichezo. |
|
Muda wa kukabidhi vyeti kwa wanamichezo. |
|
Umati wa wanamichezo ukifanya mazoezi leo viwanja vya mnazi mmoja |
|
Umati wa wanamichezo ukifanya mazoezi leo viwanja vya mnazi mmoja. |
|
Wanamichezo wa Jogging wakiigia Uwanja wa Mnazi mmoja kwa Mwembwe |
|
Wanamichezo wa Jogging wakiigia Uwanja wa Mnazi mmoja kwa Mwembwe wakionyesha utaifa kwa kuvaa fulana za Tanzania. |
Dk. Kigwangala ahimiza amani nchini
WANASIASA wameaswa kudumisha amani, upendo na mshikamano wa Tanzania, ili kuepuka vurugu zinazoweza kujitokeza ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikisababishwa na makundi ya wanasiasa, kwa kutoa ujumbe kwa wananchi unao chochea kuvurugukika kwa amani ya Tanzania.
Akizungumza na wanamichezo wa vilabu mbalimbali vya kukimbia (Jogging) kutoka Tanzania bara na Zanzibar, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, mbunge wa jimbo la Nzega, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Tawala za mikoa na seikali za mitaa, Dk. Hamis Kigwangala, amesema wakati bunge maalum la Katiba lilipokuwa likitunga katiba inayopendekezwa, kuliibuka baadhi ya wanasiasa, waliokana kushiriki katika bunge hilo na kutofautiana katika baadhi ya mambo kuingizwa katika katiba hiyo, huku wale waliobaki ndani ya bunge maalumu la katiba kwa asilimia takriban 85 wakiheshimu maamuzi ya watanzania na kuhakikisha katiba mpya inapatikana.
Hivyo amewataka wanasiasa pamoja na kuwa mapendekezo yao hayakuingia ndani ya katiba wasiwe chanzo cha kutokuridhika kwao kulazimisha na watanzania wengine wasiridhike na kwamba watanzania waachwe siku ya kuipigia kura katiba inayopendezwa itakapo tangazwa, watanzania waipigie kura ya ndio au hapana na kwamba waamue kwa utashi wao bila uchochezi wa wanasiasa.
Katika Tamasha hilo lililopewa jina la Mbio za amani 2014, Dk, Kigwangala pia amehimiza umuhimu wa kufanya michezo kila wakati, kwani michezo ni Afya, Furaha, Amani, Upendo na Ajira, huku akivitunuku vyeti baadhi ya vilabu vya Jogging kwa kushiriki katika tamasha hilo.
Tamasha hilo limeshirikisha wanamichezo wa vilabu vya Jogging kutoka Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam, ambapo limeandaliwa na Faita Jogging & Sports Club ya jijini Dar es Salaam, huu ukiwa ni mwaka wa tatu kuandaliwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.