ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 16, 2014

HALMASHAURI ZA MAJIJI NA MANISPAA ZAKEMEWA.

NDG. ZUBERI M. SAMATABA, KAIMU KATIBU MKUU- OWM-TAMISEMI AKIFUNGUA MKUTANO HUO WA SIKU TATU.
MR. ONOUR OZLY- MWAKILISHI WA BENKI YA DUNIA, ALIPOKUWA AKITOA MALEZO MAFUPI KUHUSU LENGO LA MKUTANO HUO.
JANE JACOB- MWAKILISHI WA DANIDA ALIPOKUWA AKITOA SALAM ZA DANIDA KATIKA KIKAO CHICHO.
WASHIRIKI WA MKUTANO HUO WAKIFURAHIA JAMBO WAKATI WA MKUTANO HUO.
MHANDISI EZEKIELI MAGOTI KUNYALANYALA, AKIWASILISHA MADA KATIKA KIKAO HICHO.

Na: Atley Kuni- Afisa habari  Mwanza.
 
Halmashauri za majiji na manispaa zimehimizwa kutunza na kuhifadhi miradi yote ya maendeleo inayo tekelezwa katika maeneo yao na kuhakikisha inadumu kwa manufaa ya kizazi cha leo na kijacho.
 
Kauli hiyo imetolewa mapena hivi jana na Zuberi Samataba, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza wakati wa kikao cha pamoja baina ya TAMISEMI, Benki ya Dunia (World Bank) DANIDA na watendaji kutoka halmashauri zinazo tekeleza miradi ya Tanzania Strategic Cities Project (TSCP).
 
Samataba, amesema, kuna haja kwa kila halmashauri kuhakikisha inatunza miradi yote ambayo inafadhiliwa na wahisani hata baada ya wahisani kumaliza muda wao na kuondoka  kasha  miradi hiyo mikononi mwa Halmashauri. "Nivema mkawa  mnatenga fedha kwa ajili yakuhudumia miradi inayo anzishwa na wafadhili kwa ajili ya ukarabati na kuimarisha  ili iendelee kudumu kwa muda mrefu hata baada ya miradi hiyo kuisha muda wake na wafadhili kuicha mikononi mwetu".
 
Katika hatua nyingine  amewaagiza watendaji hao kutoa taarifa kwa wakati ili kujenga imani kwa wafadhili wanao toa fedha zao kwa ajili ya miradi mbali mbali ya maendeleo wanayo ifadhili, "Wenzetu suala la mrejesho ni muhimu sana lakini zaidi sana mrejesho kwa wakati,  kwani  ni kama wanasheria wanavyo amini kuwa HAKI ILIYO CHELEWESHWA NI HAKI ILIYO NYIMWA". kwa mantiki hiyo kutoa taarifa kwa wakati ni suala muhimu sana,  vinginevyo au kinyume chake nikuwafanya wafadhili kupoteza imani kwa wanao wafadhili kwenye miradi amesema na kuongeza kuwa kwakuwa serikaliinaondoka kwenye utendaji wa kawaida na kuelekea kwenye utendaji wa upimaji ufanisi kwa matokeo (Performance for Result ) hivyo moja ya kigezo muhimu kitakachotumika ni kupima matokeo ni uwasilishaji wa taarifa kwa wakati.
 
Kikao hicho cha siku tatu kina wakutanisha Watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Halmashauri Jiji la Mwanza , Manispaa ya Ilemela, Manispaaya Kigoma Ujiji, Manispaa ya Dodoma, (CDA), Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Halmashauri ya mikindani Mtwara, Jiji la Tanga, Jiji la Arusha pamoja na wawakilishi wa DANIDA sambamba na  World Bank.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.