Wanafunzi wa shule ya Sekondari Shibula wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa halfa ya kupokea msaada wa vitabu kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel. |
Airtel yatoa vitabu kwa shule ya sekondari Shibula Mwanza
MWANZA, Jumanne 23 Septemba 2014, Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Shibula iliyoko Mkoani Mwanza wamefaidika na vitabu kupitia mradi wa Airtel shule yetu ambapo Airtel imetoa msaaada wa vitabu vya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni moja na Laki tano vitakavyo wawezesha wanafunzi hao kupata elimu bora.
Kwa zaidi ya miaka 10 sasa mpango huu wa Airtel shule yetu umekuwa ukisaidia shule za sekondari kwa kuwapatia nyenzo muhimu kma vile vitabu, vifaa za kufundishia , madawati, kuboresha majengo ya shule lengo likiwa ni kuboresha ubora katika kutoa elimu nchini.
Akiongea wakati wa hafla ya kikuabithi vitabu Meneja Mauzo wa Airtel kanda ya Ziwa Bwana Raphael Daudi alisema “ Airtel imewekeza kiasi cha kutosha katika kusaidia malengo mkakatika katika sekta ya elimu kwa kushirikiana na serikali katika kutoa elimu bora.
Kwa kupitia mradi wa Airtel Shule yetu tumeweza kuzifikia shule zaidi ya 1000 zilizoko
katika maeneo mbalimbali nchini kwa kuwapatia vifaa vya kujisomea na kupunguza changamoto za uhaba wa vitabu huku tukifanikiwa kupunguza uwiano wa kitabu kwa mtoto kutoka watoto 6 kwa kitabu kimoja hadi watoto 2 kwa kitabu kimoja.
Leo tunatoa vitabu vya masomo ya sayansi ikiwemo Hisabati Fizikia, Kemia na Baiologia kwa shule ya Shibula sekondari tukiamini utachangia katika kuongeza kiasi cha ufaulu na kuchochea wanafunzi wengi kujiunga na masomo ya sayansi. Tutaendelea na jitihada hizi katika kuboresha sekta ya elimu na kuhakikisha tunazifikia shule nyingi zaidi nchini
aliongeza Daudi.
Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ilemema Mkoani Mwanza Juma Kasandiko ameishukuru Airtel kwa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari zilizoko mwanza na kuwaasa wanafunzi kutumia muda wao kujisomea na kuacha tabia ya utoro shuleni na kwa kufanya hivyo kutasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi shuleni hapo na Mwanza kwa ujumla.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Shibula Bwana James Elias Chitanda alisema” Napenda kuwashukuru Airtel kwa kutoletea msaada huu wa vitabu shule ni hapa, vitabu ni nyenzo muhimu katika kuongeza maarifa na ujuzi hivyo vitabu hivi vitasaidia kuhamasisha wanafunzi wengi kujisomea na kuongeza upeo, vitawasadia walimu kuandaa masomo yao na kuwahamasisha wanafunzi wengi kujiunga na masomo ya sayansi na kuongeza idadi ya wanasayansi kwa ujumla.Tunatoa wito kwa makampuni mengine kujiunga na kuchangia katika sekta ya elimu kwani ina mahitaji na changamoto nyingi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.