Airtel yatoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari Dar · Zaidi ya shule 30 kufaidika na msaada wa vitabu kwa mwaka huu, kupitia mradi wa Airtel “Shule yetu” Dar es Salaam.
Jumanne 9 septamba 2014,
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa “shule yetu” umeendelea na mpango wake wa kuchangia katika kusaidia sekta ya elimu nchini ambapo leo imetoa msaada wa vitabu kwa shule 3 za sekondari jijini Dar es saalam Shule zilizofaidika na msaada huo ni pamoja na Kambagwa sekondari iliyopo wilaya Kinondoni, shule ya sekondari Mvuti iliyopo wilaya ya Ilala na shule ya sekondari Mbagala iliyopo wilaya ya Temeke ambapo kila shule imepata vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano.
Akiongea wakati wa kukabithi vitabu hivyo, Meneja huduma kwa jamii Airtel Bi Hawa Bayumi alisema” Tunayofuraha kuendelea na mpango huu wa “shule yetu” kwa mwaka huu na kuwa na shule mpya zitakazofaidika na vitabu vya masomo ya Sayansi.
Tunazo shule zaidi ya 30 ambazo tumezipata kwa kushirikiana na uongozi wa serikali zitakazofaidika na msaada huu wa vitabu kwa mwaka huu, Na leo tumeweza kuzifikia shule za Kambagwa, Mvuti na Mbagala na kuwapati vitabu vitakavyoweza kuleta tija katika ufaulu na elimu kwa ujumla”.
“Nia yetu ni kuendelea kushirikiana na Serikali chini ya wizara ya elimu katika kuinua sekta ya elimu nchini huku tukiwekea mkazo katika masomo ya sayansi kwani tuaamini ulimwengu na nchi inahitaji wanasayansi wengi ili kwenda na kasi ya ukuaji wa technologia. natoa wito kwa walimu na wanafunzi basi watumie vitabu vizuri na kuweza kuongeza wanafunzi wengi katika masomo ya sayansi na hatimae kuongeza ufaulu zaidi.aliongeza” Bayumi
Akiongea kwa niaba ya walimu wakuu wa shule zilizopokea msaada jijini Dar es saalam, Mwalimu mkuu wa shule ya Mbagala Bi Marcelina Kimaro alisema” Tunawashukuru sana Airtel kwa kutufikia leo, tumekuwa tukiona shule nyingi zikifaidiaka na mpango huu wa “Shule yetu” na leo tunayofuraha kupokea msaada wa vitabu vya Hisabati, Chemia, physikia na Baiologia kutoka Airtel Shule hii ya mbagala Sekondari ina jumla ya wanafunzi 2031 na uwiano wa vitabu kwa wanafunzi kwa sasa ni kati ya kitabu kimoja kwa wanafunzi wa 3 au 4 , kwa msaada huu leo utasaidia kupunguza changamoto tuliyonayo ya uhaba wa vitabu na kufanya uwiano kuwa kitabu kimoja kwa wanafunzi wawili.
Halikadhalika msaada huu utatupatia urahisi katika kusoma na walimu kuandaa masomo yao. Kimaro aliongeza kwa kusema” Vitabu hivi vimetupa changamoto kubwa ya kuongeza juhudi katika masomo kwani nyenzo sasa tunazo na tunaamini wanafunzi wetu wa masomo ya sayansi watasoma kirahisi na hatimaye kupata idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi.
Tunawaahidi kuvitunza na kuvitumia vitabu hivi kwa faida ya wanafunzi na jamii kwa ujumla” Chini ya mpango wa “shule yetu” Airtel imeweza kutoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari zaidi ya 1000 nchini huku mpango ukiwa ni kizifikia shule nyingi zaidi kila mwaka.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.