The picture. |
Picha ya pamja mara baada ya uzinduzi wa vilainishi vya GAPCO RELSTARALPHA 4T vya Pikipiki za miguu miwili na mitatu wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa jijini Dar es Salaaam. |
TOLEO KWA
VYOMBO VYA HABARI
Dar es
Salaam, JumatatuAgosti 4 2014: Kampuni ya Gapco Tanzania Ltd
leo hii imezindua kilainishi kipya cha pikipiki kilijulikanacho kama Relstar Alpha 4T
Ultra.
Uamuzi wa Gapco kuzindua bidhaa hii ni kutokana na ongezeko kubwa la
pikipiki nchini haswa kwa matumizi ya kibiashara.
Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi huo,
Mkurugenzi Mkuu wa Gapco, Bwana. Macharia Irungu alisema,
“Utafiti umetuonyesha kwa sasa watumiaji wamiliki wengi wa pikipiki wanalazimishwa kutembelea gereji mara mbili kwa mwezi kwa ajili ya kurekebisha pikipiki zao.
Kupitia kilainishi chetu cha Relstar Alpha 4T Ultra
tunawahakikishia wateja wetu kutumia muda mfupi kwenye warsha na kupata maili zaidi kwa pesa zao.
Ongezeko kubwa
la pikipiki au bodaboda nchini limeleta pia ongezeko la
vilainishi vya pikipiki vyenye viwango vya chini. Kupitia kilainishi kipya cha
Gapco wateja wataweza kupata;
maili zaidi na akiba wanapoenda kufanya marekebisho kwenye pikipiki zao.
Naye Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,
Kamanda waTrafiki, Bwana. Mohamed Mpinga aliwaonya watumiaji wa pikipiki kuepuka na na vilainishi vya viwango vya chini na pia kuwahimiza kutii sheria za barabarani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.