ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 2, 2014

GUILLERMO OCHOA NI UVUMI KUWA YEYE NI KIPA MWENYE VIDOLE SITA..??

Picha ya leo kwenye vyombo vya habari ina mwonyesha golikipa huyo akiwa na vidole sita, Jeh ni kweli au imefanyiwa manuva kama ile inshu ya picha za falagha za Kapteni JK?
 Fortaleza, Brazil. Inawezekana kuwa Mexico imetolewa ‘kikatili’ kwenye hatua ya 16 bora ya fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil. Visa vya winga wa Uholanzi, Arjen Robben kujiangusha na hatimaye kupata mkwaju wa penalti vilikatisha safari ya Mexico.
Hata hivyo, wakati ikirejea Mexico City, timu hiyo imeacha simulizi kubwa kwenye fainali hizo, na hasa juu ya umahiri wa kipa Guillermo Ochoa langoni.
Ochoa, ambaye ana umri wa miaka 28, aliwazuia washambuliaji wengi kutikisa nyavu zake, wakiwamo wa Brazil walioongozwa na Neymar katika mchezo ulioisha kwa timu hizo kutofungana.
Kipa huyo alikuwa kizingiti kwenye lango la Mexico, majarida mengi duniani likiwemo gazeti la MWANANCHI yamediriki hata kusema kuwa ana kitu cha ziada; Hilo halina 'Ubishi' lakini jeh pale wanaposema kuwa golikipa huyo ana vidole sita kweye mkono wake  wa kulia ni sahihi? Hebu fuatilia kwa umakini picha zake halisi zifuatazo.
Picha halisi ya awali ambayo ilichakachuliwa na hatimaye kupata picha yenye vidole sita.
Picha za Kipa huyo akiwa airport akiwapungia mashabiki wake huku akitumia mkomo ule ule wa kulia unaotajwa kuwa una vidole sita.
Hata akiwa langoni?
Ochoa, mwenye umri wa miaka 28 ambaye msimu ujao hana timu badala ya klabu yake ya sasa Ajaccio ya Ufaransa kutompa mkataba mpya, alikuwa kivutio kwa mashabiki wa nchi hiyo kiasi cha wengine kumwita “rais”
Ameichezea klabu hiyo mechi zaidi ya 100. Umahiri wake langoni utaweza kumpatia timu.
Hakuna shaka, klabu za barani Ulaya kama Arsenal na Manchester City zimevutiwa naye, ingawa yeye anapenda kubakia Ufaransa.
Safari yake ya kwenda Ufaransa mwaka 2011 ilikumbwa na kiwingu baada ya kuhusishwa na matumizi ya dawa za kulevya. Alikuwa miogoni mwa nyota watano waliokumbwa na kashfa hiyo. Alitiwa hatiani kwa kutumia dawa aina clenbuterol na kufungiwa.
NA G.SENGO/GAZETI LA MWANANCHI 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.