FAINALI
za mashindano ya Ngoma za Asili ngazi ya mikoa zijulkanazo kama “Balimi Ngoma Festival
2014”
Tabora na Shinyanga wamepata wawakilishi watakao wakilisha mikoa hiyo katika fainali za
Kanda ya Ziwa zinazotarajiwa kufanyika Augusti 16,2014, Mkoani Mwanza.
Mkoa wa Tabora kikundi cha Magereza Arts Group
kilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mkoa huo na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi
600,000/=
na tiketi ya kuwakilisha kwenye fainaliza Kanda. Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha
Bugobogobo na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 500,000/=
pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za Kanda.
Jumla ya vikundi 8 ambavyo ni pamoja na JKT, Hekima, Uvikuja, Wembe Group, Hiariya Moyo, Zugo
Group. Mkoa wa Shinyanga kikundi kilichofanikiwa kuchukua Ubingwa ni Mabulo ya Jeshi ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi
600,000/=
pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Shinyanga kwenye fainali za Kanda. Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi
cha Wananguli Bugumbagu ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 500,000/=
pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Shinyanga kwenye fainali za Kanda Mkoani Mwanza. Jumla ya vikundi
10
Shinyanga vilishiliki ambavyo ni pamoja na Wagoyangi Bugumbagu, Buzori Usule, Bagoyangi Usule, Busumbi, Kadete Chibe, Wagoyangi Maswa, Wananguli Bugimbaguna Uswezi Usule.
Akizungumza na kwanya kati tofauti Meneja matukio wa Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela alisema Sababu ya msingi
ya kuwepo kwa Mashindano ya Balimi Ngoma za Asili ni kuenzi na kulinda
utamaduni wa Kitanzania.
Mwayela aliongeza
pia kuwa wao Kampuni ya Bia nchini ni sehemu yao ya kurudisha fadhila kwa
watumiaji wa Kinywaji cha Balimi Extra Lager pamoja na vinywaji vyote vya
Kampuni ya Bia Tanzania(TBL).
Fainali za Kanda
za mashindano ya Balimi Ngoma zinatarajiwa kufanyika August 16,2014 jijini
Mwanza kwa kushilikisha vikundi viwili viwili kutoka Tabora, Shinyanga,
Bukoba, Musoma na Wenyeji wa mashindano
Mwanza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.