ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 24, 2014

PICHA ZA WAZIRI MEMBE ALIVYO ZINDUA KWA KISHINDO FILAMU YA 'I LOVE MWANZA' UWANJA WA CCM KIRUMBA.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (kushoto) akionyesha zao la kwanza la filamu ya I Love Mwanza aliyoizindua katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, kulia ni Rais wa Shirikisho la filamu nchini Tanzania Saimon Mwakifamba.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akiwapungia mkono kama salaam wananchi waliofurika kwa wingi uwanja wa CCM Kirumba kushuhudia zao la kwanza la filamu ya I Love Mwanza, Membe amehudhuria tukio hilo kuchagiza wananchi kupenda vya nyumbani na kuvithamini.
Watu wameitikia wito na mahudhurio yametikisa.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akipata picha na mmoja kati ya watoto walioomba kupata kumbukumbu naye kutoka kwa familia ya baba anayeonyesha uchangamfu pichani.
Watu wamejiachia kwa raha zao.
Mc Namba moja mwanamuziki wa muziki asili nchini Mrisho Mpoto aka 'Mjomba'.
Twanga Pepeta walisababisha katika sekta ya burudani.
Twanga Pepeta inajivunia vijana wawili wanaotoaka kanda ya Ziwa mmoja ni Dogo Rama mwingine ni huyu Mwana  Mwanza Kwanza Jeh....wamjua kwa jina?
Mc Namba mbili.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (katikati) kabla ya kuhutubia umma wa wananchi waliofurika kumuunga mkono katika uzinduzi wa zao la kwanza la filamu ya I Love Mwanza aliyoizindua katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza,
Mpoto akipasuka kwenye kipaza...!!!
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe amewaasa wananchi na wasanii kupigana kufa na kupona kuhakikisha vita dhidi ya maharamia wa Filamu nchini inadumishwa ili kuwakosesha mwanya maharamia hao wa kujiachia na kudurufu kazi zao bila idhini. "Wananchi kataeni kununua kazi za wizi zingatieni zile original zenye nembo za kiusalama zilizo thibitishwa, wezi wanawaibia wasanii wetu kwa sababu tunawasapoti kwa kununua kazi feki" Akisisitiza kuwa vita hiyo ni ya kila Mzalendo, mwenye mapenzi mema na aliye na uchungu wa Taifa. 
Hapa Bongo Movie walifanya yao.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akionyesha zao la kwanza la filamu ya I Love Mwanza aliyoizindua katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza,
Na kule waone....!!
Watu wameitika bana...!!
Mratibu wa Wasanii kupitia Shirikisho la Filamu Kanda ya Ziwa Hussein Kimu akiwa amebebwa juu na wapambe wa Kampuni wadhamini wa tukio hilo Coca cola mara baada ya kuitwa jukwa kuu.
Mweyekiti wa Bongo Movie Nchini Steve Nyerere alichomoja toka jukwaani na kwenda moja kwa moja hadi jukwaa la Twanga Pepeta kuwatunza wanamuziki hao.
Huku akishangiliwa kwa sauti zivumazo kwa kishindo Jb naye hakuwa nyuma....
Mweyekiti wa TDFAA Mwanza Bi. Anita Kagemulo akiwa juu.....!!!
Watu tukioni.
Makhirikhiri toka Kanda ya ziwa nao walikuwepo.
The Crew.
Hongera Waziri Membe kwa kukubali kusapoti filamu mkoa wa Mwanza, Hongera wananchi wa Mwanza kwa kuitikia wito na kujitokeza kwa wingi tukioni kununua Filamu ya vijana wenu.
I Love Mwanza,
I Love Tanzania. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.