ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 26, 2014

BAADA YA MAOMBELEZO YA KIFO CHA SWAHIBA WAO IRAKI HUDU (RIP) FFU wa NGOMA AFRICA BAND WAPANDA TENA JUKWAANI UGHAIBUNI !

Ngoma Africa Band aka FFU,aka Viumbe wa ajabu Anunnaki alimaaru watoto wa Mbwa wakiwa kazini.
Mkaanga Chips wa FFU Sgt.JO JO Souza akikaanga vitu.
Mmojawapo ya vijana wa FFU na Mtutu wake.
Mshambuliaji FFU Matondo akimimina makombora ya machozi kwa washabiki.
Ngoma Africa Band aka FFU,wakiwa jukwaani tena katika Datzenbach Festival.
Frankfurt,Ujerumani.
Bendi ya Muziki wa dansi Ngoma Africa band alimaarufu  " FFU-Ughaibuni"  walipanda tena jukwaani jumamosi ya 21 Juni 2014 katika Ditzenbach Festival,nje kidogo ya mji wa Frankfurt,kule Ujerumani.

Bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya yenye makao yake nchini Ujerumani ilikuwa katika maombolezo ya siku saba kutokana na kifo cha layekuwa Swahiba wao wa karibu bondia mkongwe hayati IRAKI HUDU aka Kimbunga(RIP) ambaye alifariki 13.juni 2014 mjini Dar-es-salaam. Baada ya maombolezo hayo bendi hiyo sasa inaendelea na taratibu zake za maonyesho huko ughaibuni.

wasikilize ffu-ughaibuni at www.ngoma-africa.com  au http://www.ngoma-africa.com   

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.