ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 31, 2014

USIKU WA LEO VILLA PARK KUNALIPUKA SHANGWE NI MALAIKABAND LIVE.



 BOFYA PLAY KUSIKIA MPANGO MZIMA.


BENDI ya muziki wa dansi ya Malaika yenye masikani yake jijini Dar es salaam, leo Mei 31 iko jijini Mwanza kwa ajili ya kutoa burudani kwa mashabiki wa jiji hilo.

Mratibu wa ziara hiyo, Meneja wa burudani wa Villa Park Resort Ramadhan Maganga alieleza kuwa, ziara ya Bendi hiyo imeratibiwa kwa pamoja na Villa Park Resort ya jijini Mwanza na Alpha Hoteli ya mkoani Geita, ratiba ya ziara hiyo imeanza jana Mjini Geita Mei 30.

“Wakazi na mashabiki wa Mji huo hakika wameshuhudia sauti yenye mvuto ya mwimbaji mahiri Christian Bela na kundi zima la wanamuziki wa Malaika bendi lakini pia wamepata fursa ya kuzisikia live nyimbo zao na ufundi wa wapigaji vyombo na wacheza show wakali bila kumsahau Rapa mkali Totoo ze Bingwa pale ndani ya Omega Resort,” amezungumza tena meneja huyo.

Maganga amesema leo jumamosi ya Meii 31 2014 ni zamu ya wakazi na mashabiki wa Jiji la Miamba ya Mawe (Rock City) ambapo bendi ya Malaika itatoa burudani ya uhakika ndani ya Villa Park Resort ambapo Bela ambaye hujiita Rais wa Vijana atafanya makubwa.

“Bela atautambulisha live kwa kuimba wimbo wake mpya unaotamba kwa sasa katika Radio, TV na Kumbi za burudani wa “Nani kama Mama” lakini pia atawashukuru kwa kuwaonyesha mashabiki wa muziki wa dansi Tuzo yake aliyoipata hivi karibuni ya Kilimanjaro Music Award (KMA) 2014 lakini wakiwa Villa watasindikizwa na Bendi ya Super Kamanyola ya jijini Mwanza,” alieleza.

Aidha baada ya jijini Mwanza, bendi ya Malaika itahitimisha ziara yake Kanda ya Ziwa kwa burudani ya kufa mtu katika Mji wa kibiashara na Madini wa Kahama katika Ukumbi wa Social Club ambapo itakuwa ni mara ya kwanza kabisa kufanya ziara yake hiyo kwa Mikoa hii.

Wito wangu kwa wananchi na mashabiki wa muziki wa dansi wasikubali kusimuliwa bali wafike kujionea burudani ya uhakika kutoka kwa wanamuziki wa bendi hiyo ambapo katika maeneo yote watakayotoa burudani mashabiki watalazimika kulipia kingilio cha Sh. 10,000/= tu, ulinzi wa mali utaimalishwa kwa asilimia 100 hivyo hakutakuwa na usumbufu wowote na watoto chini ya miaka 18 hawataruhusiwa kuingia kwenye show hizo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.