Kutoka kushoto ni Joh Makini, Richie Mavoko, Laban Mbibo aka Dabo 'The Energy God',na Young Killer wakiwa meza moja kuzungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Mwanza |
Mkali wa muziki wa Africa Mashariki mwanadada Mwasiti Almasi ametoa ahadi kwa mashabiki wake kutoa burudani yenye utofauti 'full kiwango' kwani kila siku sanaa yake amekuwa akiiongezea kitu kipya. |
Richie Mavoko. |
Nikki wa Pili (L), Mwasiti (R). |
Kutoka kushoto ni Mwasiti Almasi, Ommy Dimpoz, Ben Paul, G. Nacko, Young Killer na mkali wa Ragga Dabo. |
Tyme ya Ommy Dimpoz kuzungumza na wanahabari. |
Richie Mavoko (L) na Joh Makini (R). |
Tayari joto la show hiyo limeshaanza kwa Promosheni mbalimbali natayari imeanza kuleta msisimko mkubwa kwa wakazi wa Rock City huku waadhamini, Kilimanjaro Premium Lager wakiwaahidi wakazi wa Mwanza mambo makubwa zaidi.
Wasanii watakaoipamba show hiyo tayari wako jijini Mwanza ambaoni pamoja na Ommy Dimpoz, Izzo Biznes, Christian Bella, Fid Q, Weusi (Joh Makini, Niki wa Pili, G. Nako) Mwasiti, Young Killer, Vanessa Mdee na Richie Mavoko.
Meneja wa Bia ya kilimanjaro Premium Lager amesisitiza kuwa hii siyo ziara ya washindi a Tuzo za Mziki za Kilimanjaro (Kili Music Awards), bali ni ziara ya kuwasaidia wasanii kutangaza kazi zao mikoani.
"Huwezi kupeleka kila mtu lakini tumejitahidi kuwachukuwa wasanii mbalimbali ili wapelekeburudani mikoani na waweze kutangaza kazi zao" alisema.
Ameongeza kuwa baada ya wakazi wa Moshi kuipokea vizuri ziara hiyo, ni matarajio ya Kilimanjaro Premium Lager kuwa show ya Mwanza itakuwa kubwa zaidi. "Baada ya kutoka Mwanza,ziara hii itaelekea Kahama Juni 7, Kigoma Juni 14, Iringa Juni 21, Mbeya Agosti 9, Dodoma Agosti 16, Tanga Agosti 23,Mtwara Agosti 30, Dar es Salaa September 6"
Kaulimbiu ya mwaka huu ni 'Zungusha Kikwetukwetu'
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.